RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

MWILI WA LIYUMBA WAAGWA JIJINI DAR

Gari lenye mwili wa marehemu ,Amatus Liyumba ukiwasili leo mchana Nyumbani kwake Mikocheni jijini Dar.
Jeneza lenye mwili wa marehemu likishushwa kwenye gari tayari kwa ajili ya kuingizwa nyumbani kwake.


Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Global Publishers, Eric Shigongo ( watatu kushoto) akishiriki kubeba jeneza lenye mwili wa Marehemu, Amatus Joachim Liyumba nyumbani kwake mikocheni.

Picha ya marehemu enzi za uhai wake.


.Baadhi ya wanafamilia wakiomboleza msibani hapo.

Wanakwaya waliotumbuiza msibani hapo.

Jeneza lenye mwili wa marehemu,Liyumba.



Padri wa Kanisa la Mtakatifu Michael, Kawe jijini Dar, Fr. Nicholas Kundyaj akiendesha ibada fupi msibani hapo.

Baadhi ya waombolezaji wakipita pembeni ya jeneza kutoa heshma za mwisho.

Wakiendelea kutoa heshima za mwisho

HATIMAYE mwili wa aliyekuwa Mkurugenzi na Utumishi wa Benki Kuu ya Tanzania ( Bot), Amatus Liyumba, leo umeagwa katika nyumba yake iliyopo Mikocheni B, jijini Dar.

Akizungumza na GPL, mpwa wa marehemu, Arbogasti Chiwembo, alisema marehemu mjomba wake alifariki Aprili 18,

mwaka huu katika Hospitali ya Agha Khan kutokana na maradhi ya kisukari na shinikizo la damu. Ameacha watoto saba na mwili wake utasafirishwa kesho alfajiri kuelekea Mahenge mkoani Morogogo kwa ajili ya mazishi.

Marehemu Liyumba aliwahi kukabiliwa na kesi ya matumizi mabaya ya ofisi kati ya mwaka 2001 na 2006 wakati wa ujenzi wa majengo pacha ya makao makuu ya BoT, ambapo alifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa kuisababishia serikali hasara ya Shilingi bilioni 221.

Habari :Gabriel Ng`osha na Denis Mtima/GPL

Comments