TANGAZO MUHIMU

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BISHOP DR. M.E. ADMIN

BISHOP DR. M.E. ADMIN

SANDLANDS HOTEL KARIAKOO

NDOTO YA TUMAINI NJOLE YASABABISHA WAUMINI WA KANISA LA MLIMA WA MOTO MIKOCHENI "B" KUKIMBILIA MADHABAHUNI KUMSHIKA MKONO BISHOP DR. GETRUDE RWAKATARE

Siku ya Jumapili 17.04.2016 ni mwimbaji wa nyimbo za Injili Tanzania Tumaini Njole anayetamba kwa wimbo wake wa “Sema na Yesu” aliweza kuhudumu katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni “B” jijini Dar es Salaam. Akiwa madhabahuni aliweza kuelezea ndoto aliyoota na baadae aliimba. Wakati wa kuelezea ndoto yake watu waliweza kumiminika madhabahuni kwenda kumshika BISHOP wa kanisa hilo Dr. Gertrude Rwakatare. Soma alichokizungumza siku hiyo . Ni heshima yangu kubwa kwa mama yangu hapa, Bishop Gertrude Rwakatare Ilikuwa niimbe wimbo wangu wa fire, fire, lakini nikiwa naomba usiku, niliona naleta sadaka kwa Bishop Dr. Gertrude, na wakati naleta sadaka niliona wanawake wengi wakileta sadaka kwa Bishop, na wakati naweka sadaka, kulikuwa kuna mtu pembeni anagawa zawadi kwa wale wamama waliokuwa wanaleta sadaka pamoja na mimi, wakati ninasimama nikaona ninaimba,

’Hakuna lisilowezekana kwa Yesu, yote yanawezekana’’

Tumaini Njole

Nilikuwa ninasikia huo wimbo unaimbwa. Kwahiyo ninaomba wanawake wote ambao mko tayari kushiriki zile Baraka nilizoziona usiku, usimame mahali ulipo uje tumbariki Bishop wetu mzuri, huyu ni mama aliyebarikiwa Afrika Mashariki. Hatuna mama kama huyu, nataka nikwambie Baraka zako ziko Mlima wa Moto Mikocheni “B”. “Neno la Nabii ni Sheria”. Mwanamke yeyote unayenisikia leta sadaka yako ya upendo. Nimeona watu wakipokea, nimeona wanawake wanapewa zawadi na mtu aliyesimama pembeni ya mama. Sijui unanielewa ewe mwanamke uliye hapa ibadani. Karibia mahali hapa upokee kwa maana iko neema mchana huu wa leo. Katika ndoto yangu niliona mtu akigawa zawadi na wimbo nilioupanga kuimba haukuimbwa, Haijalishi una mzigo mkubwa namna gani, haijalishi una mateso ya namna gani, haijalishi unapitia laana na taabu kwani iko neema mchana huu wa leo. Biblia inasema, “Yeye alihamishwa na kufungwa atafunguliwa haraka”, Ninasema na wewe mwanamke, ninasema na wewe binti, nasema na wewe uko mahali unasikia ni saa yako ya kupokea, iko neema ya kupata zawadi yako nzuri. Umefunga na kuomba lakini saa hii ni saa ya muujiza wako, Usipoteze nafasi yako, usipoteze maombi uliyoomba na kufunga kwa siku tatu. Asante Yesu.


0