RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

NIMEPOKEA TAARIFA MPYA ZA UTEUZI KUTOKA IKULU LEO APRIL 25 2016

April 25 2016 imetolewa taarifa kutoka Ikulu kupitia kwa Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi ambayo imeeleza kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli amemteua Kamishna wa Polisi Thobias Andengenye kuwa Kamishna Mkuu wa Jeshi la Zimamoto nchini. 

Kamishna wa Polisi Andengenye anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Mhandisi Pius Makuru Nyambacha ambaye amestaafu. Kabla ya uteuzi huo Kamishna wa Polisi Thobias Andengenye alikuwa Kamishna wa Utawala na Utumishi, Makao Makuu ya Jeshi la Polisi, uteuzi wa Kamishna Andengenye umeanzia leo tarehe 25 Aprili, 2016.

Wakati huo huo, Rais Magufuli amemteua Donan Mmbando kuwa Mtendaji Mkuu wa Hospitali ya Benjamin Mkapa ya Dodoma.

Comments