RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

PICHA: DARAJA LA KIGAMBONI LAANZA KUTUMIKA


IKIWA zimebaki siku mbili tu ili Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli azindue rasmi Daraja la Kigamboni lenye urefu wa mita 680 ambalo limejengwa juu ya Bahari ya Hindi kuunganisha kata za Kigamboni na Kivukoni, mapema hii leo wananchi wameonekana wakitumia daraja hilo kuvuka kutoka upande mmoja kwenda mwinguine ambapo pia magari yameonekana yakipita.

Daraja hilo ambalo limejengwa katika mkondo wa Kurasini (Kurasini Creek), mradi huu uliobuniwa na Arab Consulting Engineers na kujengwa na wakandarasi kampuni za China Railway Jiangchang Engineering (T) Ltd na China Major Bridge Engineering Company, unamilikiwa na Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF).

Sherehe za uzinduzi rasmi wa daraja hilo utafanyika Jumanne ijayo huku mgemi rasmi atakayezindua daraja hilo atakuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.
Mwananchi akipita kwenye daraja la Kigamboni.
Mtangazaji wa Global TV Online, Adria Cleophace akimhoji mmoja wa watumiaji wa daraja hilo.
Watumiaji wakielezea namna ambavyo watanufaika na utumiaji wa daraja hilo. 
Mama ndani ya gari lake akionekana mwenye furaha kuvuka daraja la Kigamboni.


Hali halisi ilivyo kwenye daraja hilo.
Taswira kamili.
Magari na watembe kwa miguu wakivuka.

Bodaboda nazo zikitumia daraja hilo.

Eneo la maegesho ya magari binafsi.
Wakina mama watembea kwa miguu wakivuka.


Eneo la maegesho ya magari.

Comments