RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

RAIS MAGUFULI KUSAFIRI NJE YA NCHI KWA MARA YA KWANZA KESHO, ANAONDOKA NA GARI SIO NDEGE

Rais wa awamu ya tano wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dk John Pombe Magufuli, April 5 2016 jina lake limerudi kwenye headlines kwa mara nyingine tena. Rais Magufuli amerudi kwenye headlines baada ya kukubali mwaliko wa Rais Paul Kagamewa Rwanda, hivyo atafanya ziara ya siku mbili Jumatano na Alhamisi.

Stori kutoka wizara ya mambo ya nje zinaeleza kuwa Rais Magufuli pamoja na RaisKagame watafungua daraja la kimataifa la Rusumo linaounganisha mpaka wa Tanzaniana Rwanda na kuzindua ushirikiano wa huduma za kituo cha pamoja.Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na vyombo vya habari na kusomwa katika television za Tanzania RaisMagufuli atasafiri kwa gari.
Kutoka kushoto ni Rais Magufuli na Rais Paul Kagame wa Rwanda

Rais Magufuli pia atakwenda kuweka shada katika makaburi ya mauaji ya Kimbali ya mwaka 1994 na baadae kufanya mazungumzo ya pamoja na Rais Kagame mjini Kigali. Hii ndio itakuwa safari ya kwanza ya Rais Magufuli kusafiri nje ya nchi toka aingie madarakani October 2015.

Comments