MelK Premium Suits

TANGAZO MUHIMU

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BISHOP DR. M.E. ADMIN

BISHOP DR. M.E. ADMIN

SANDLANDS HOTEL KARIAKOO

ROBOTI WA KIKE ATENGENEZWA CHINA

UNAWEZA kushangaa lakini ndiyo ukweli wenyewe kwamba jamaa mmoja anayejulikana kwa jina la Chen Xiaoping amefanikiwa kutengeneza roboti wa kike na kumpa jina la Jia Jia lenye maana ya mungu roboti wa kike.

Chen Xiaoping anasema kwamba kwa kipindi kirefu amekuwa akiwaona watu wakitengeneza maroboti wenye vyuma hivyo alichokuwa akifikiria ni kutengeneza roboti na kisha kumvisha ngozi, aonekane kama binadamu, na kweli akafanikiwa kwa asilimia kubwa.

Ukimwangalia roboti huyu, ni vigumu kumgundua kwani ana kila kitu kwa nje ambacho binadamu wa kawaida anacho. Lengo lake la kutengeneza roboti huyo hakusema, kama ni kufanya kazi au vitu vingine ila kitendo cha kutengeneza roboti huyo kimempa heshima kubwa kijana huyo aliyekuwa akisoma katika Chuo cha Sayansi na Teknolojia hapohapo China.
Roboti wa kike (kulia mwenye nguo nyekundu) aliyetengenezwa na Chen Xiaoping na kumpa jina la Jia Jia lenye maana ya mungu.


Wanahabari wakiongea na roboti huyo.


Wanahabari wakimpiga picha.


Source: Daily Mail, England.
0