RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

SOMO: PANUA MPAKA WAKO - ASKOFU JOSEPHAT GWAJIMA


JOSHUA 1: 1 “Ikawa baada ya kufa kwake Musa, mtumishi wa Bwana, Bwana akamwambia Yoshua, mwana wa Nuni, mtumishi wa Musa, akasema, Musa mtumishi wangu amekufa; haya basi, ondoka, vuka mto huu wa Yordani; wewe na watu hawa wote, mkaende hata nchi niwapayo wana wa Israeli. Kila mahali zitakapopakanyaga nyayo za miguu yenu, nimewapa ninyi, kama nilivyomwapia Musa. Tangu jangwa hili na mlima huu, Lebanoni, mpaka mto ule mkubwa, mto wa Frati, nchi yote ya Wahiti, tena mpaka bahari ile kubwa upande wa machweo ya jua, hapo ndipo patakapokuwa mpaka wenu. Hapatakuwa mtu ye yote atakayeweza kusimama mbele yako siku zote za maisha yako; kama nilivyokuwa pamoja na Musa, ndivyo nitakavyokuwa pamoja na wewe; sitakupungukia wala sitakuacha. Uwe hodari na moyo wa ushujaa, maana ni wewe utakayewarithisha watu hawa nchi hii niliyowaapia baba zao ya kwamba nitawapa. Uwe hodari tu na ushujaa mwingi, uangalie kutenda sawasawa na sheria yote aliyokuamuru Musa mtumishi wangu; usiiache, kwenda mkono wa kuume, au wa kushoto, upate kufanikiwa sana kila uendako. Kitabu hiki cha torati kisiondoke kinywani mwako, bali yatafakari maneno yake mchana na usiku, upate kuangalia kutenda sawasawa na maneno yote yaliyoandikwa humo; maana ndipo utakapoifanikisha njia yako, kisha ndipo utakapositawi sana. Je! Si mimi niliyekuamuru? Uwe hodari na moyo wa ushujaa; usiogope wala usifadhaike; kwa kuwa Bwana, Mungu wako, yu pamoja nawe kila uendako.”

Siku ya pasaka ni siku ya kusheherekea kufufuka kwake Bwana wetu Yesu Kristo, kwa kawaida huwa hatusheherekei kuteswa na kufa kwake Yesu kwasababu kuna watu walioteswa kuliko yeye kwa kuchomwa moto, kupigwa mawe na kuchinjwa hadi kufa, kila tukisema tunasheherekea kufa basi haina maana sababu kila mtu mtu amezaliwa na siku moja atakufa, ndiomaana siku ya Pasaka ni siku maalum ya kusheherekea kufufuka kwake Yesu kwasababu hakuna mtu mwingine ambaye ameshafufuka kama alivyofufuka Bwana Yesu Kristo.

Wana wa Israeli waliondoka Misri kuelekea nchi ya Ahadi wakiongozwa na Musa lakini Musa hakufika kwenye nchi ya ahadi, alifia kwenye mto Yordan na Yoshua akachukua nafasi yake kuwaongoza wana wa Israeli kuingia kwenye nchi ya ahadi, kabla hawajaingia kwenye nchi hiyo Mungu aliwapa mipaka yao, Mungu alitaka kwamba wajue mipaka yao ili wasije wakajikuta wamemiliki kumbe wamemiliki zaidi au hawajamiliki kama walivyopewa. 

Ukisoma Biblia utaona kwa Leo hii wana wa Israeli walitakiwa wamiliki Lebanoni yote, Syria yote mpaka Iraq yote lakini wao walimiliki kidogo mahali ambapo wapo hadi sasa, hii inatuonyesha kwamba tumepewa uwezo wa kumiliki sana lakini hatumiliki vile tulivyopewa kwasababu mbalimbali. Unapojua umeingia kwenye wokovu kuna mipaka ya kumiliki unayopewa na ili uweze kumiliki na njia pekee ya kumiliki ni lazima upigane na kupambana kiroho ndipo utamiliki ipasavyo. 

Mungu ni Mungu wa mipaka, Mungu amekupa ahadi nyingi kweli lakini wewe ndio unatakiwa kupenya katikati ya giza lililo mbele yako japo ni ngumu kukipata kile ulichoahidiwa lakini unatakiwa upenye japokuwa kuna moto chini, japo kuwa kuna milima wewe unatakiwa ujue kuwa Mungu ameshakuahidi ahadi nyingi hivyo ni jukumu lako kupigana na kuendea kuzidai hizo ahadi ili uzimiliki.

Ayubu 14: 1 “Mwanadamu aliyezaliwa na mwanamke Siku zake za kuishi si nyingi, naye hujaa taabu. Yeye huchanua kama vile ua, kisha hukatwa; Hukimbia kama kivuli, wala hakai kamwe. Nawe, je! Wafumbua macho yako kumwangalia mtu kama yeye, Na kunitia katika hukumu pamoja nawe? Ni nani awezaye kutoa kitu kilicho safi kitoke katika kitu kichafu? Hapana awezaye. Kwa kuwa siku zake zimeamriwa, hesabu ya miezi yake unayo wewe, Nawe umemwekea mipaka yake asiyoweza kuipita”

Ayubu anatuelezea kwamba hata mwanadamu ana mipaka yake ambayo akishafika hawezi kuivuka. Kuna watu ambao wanaishi kwa kuona kwamba wamefikia mwisho wa mipaka yao lakini upo uwezo wa kupanua mpaka na mtu akastawi zaidi na kuishi maisha marefu.

1 Mambo ya nyakati 4:” Naye Yabesi alikuwa mwenye heshima kuliko nduguze; na mamaye akamwita jina lake Yabesi, akisema, Ni kwa sababu nalimzaa kwa huzuni. Huyo Yabesi akamlingana Mungu wa Israeli, akisema, Lau kwamba ungenibarikia kweli kweli, na kunizidishia hozi yangu, na mkono wako ungekuwa pamoja nami, nawe ungenilinda na uovu, ili usiwe kwa huzuni yangu! Naye Mungu akamjalia hayo aliyoyaomba.”

Yabesi alizaliwa mwenye huzuni nyingi, lakini alimcha Bwana mpaka alifika wakati akamwomba Bwana apanue mipaka yake na Bwana alimpa haja yake. Alianza kwa huzuni lakini alimaliza mwenye heshima kuliko ndugu zake. 

Isaya 54: 1 Imba, wewe uliye tasa, wewe usiyezaa; paza sauti yako kwa kuimba, piga kelele, wewe usiyekuwa na utungu; maana watoto wake aliyeachwa ni wengi kuliko watoto wake yeye aliyeolewa, asema Bwana. Panua mahali pa hema yako, na wayatandaze mapazia ya maskani yako; usiwakataze; ongeza urefu wa kamba zako; vikaze vigingi vya hema yako. Kwa maana utaenea upande wa kuume na upande wa kushoto; na wazao wako watawamiliki mataifa; wataifanya miji iliyokuwa ukiwa kukaliwa na watu. Usiogope; maana hutatahayarika; wala usifadhaike; maana hutaaibishwa; kwa kuwa utaisahau aibu ya ujana wako, pia mashutumu ya ujane wako hutayakumbuka tena. Kwa sababu Muumba wako ni mume wako; Bwana wa majeshi ndilo jina lake; na Mtakatifu wa Israeli ndiye Mkombozi wako; Yeye ataitwa Mungu wa dunia yote.”

Huyu anayeongelewa ni kijana ambaye kuna jambo limefanyika limempeleka awe wa aibu mpaka amejiweka maisha yake yawe ya aibu lakini Mungu amesema kwamba ataisahau aibu ya Ujana wake. Mungu ndiye mkombozi wako yeye peke yake ndiye awezaye kukuokoa na kukuvusha salama.

Biblia imesema kwamba wale wamngojeao Bwana watapaa juu kama Tai,

Ayoub 24: 2 “Wako waziondoao alama za mipaka; Huyachukua makundi kwa jeuri na kuyalisha.”

Wako waondoao alama za mipaka kwenye maisha na familia yako na hao ndio wanaipindisha kesho yako. Mungu hana upendeleo bali amempa kila mtu mpaka wake sawa sawa bila upendeleo. Biblia inasema mtu mwenye haki ataishi awaone watoto wa wajukuu zake, watu ambao wanaishi kwa wasiwasi ni kwasababu wameondolewa mipaka yao ya kuishi muda mrefu hivyo wanaishi kwa kuomba maombi ya kujiepusha na kifo, wanaishi maisha ya hofu kwasababu mipaka yao ya kuishi miaka mingi imesogezwa karibu hivyo wanajiona wako karibu kumiminwa na kuanza kuongea maneno ya kuaga. Hizo ni alama za mipaka.

Mathayo 17: 26 “Naye aliposema, Kwa wageni, Yesu alimwambia, Basi, kama ni hivyo, wana ni mahuru. Lakini tusije tukawakwaza, enenda baharini ukatupe ndoana, ukatwae samaki yule azukaye kwanza; na ukifumbua mdomo wake utaona shekeli ichukue hiyo ukawape kwa ajili yangu na kwa ajili yako.”

Mungu ni Mungu wa mipaka na hii ni lugha ya rohoni ambayo inatuonysha kuwa kila mtu anao mpaka wake wa kuishi

Zaburi74: 4 “Watesi wako wamenguruma kati ya kusanyiko lako; Wameweka bendera zao ziwe alama. 
Mithali 22: 28 “Usiiondoe alama ya mpaka wa zamani, Uliowekwa na baba zako.“

Maana yake ni kwamba Tangu siku ulipozaliwa Mungu alikupa mpaka wako wakuishi, kuzaa na kuongezeka, kumiliki mpaka utakaporudi kwake. Unapokuwa katika ulimwengu wa rohoni inajulikana utakuwa nani baadaye. 

Kwenye maisha ya mafanikio ipo vilevile. Kwenye Ufunuo imeandikwa ikifika wakati Fulani, Malaika aliyefungwa afunguliwe. Hata kwenye maisha ya kawaida inaajulikana kwamba wapo wafungao. 

Wale mamajusi wachawi wa mashariki walipoiona ile nyota ya Yesu Kristo mashariki waliifuata kwasababu walijua alama ya mpaka wake, Wachawi wanaloga na wakiwa wanakwenda kuloga hawaendi na miili yao bali hutoka kiroho pamoja na roho ya uchawi na huwa na uwezo wa kuangalia alama ya mpaka wako na kuirudisha nyuma. Inawezekana ikawa mpaka wa ndoa wanaweza kuichengesha isitokee, mpaka wa safari za kibiashara zikafungwa zisitokee kwasababu tu hawapendi ufanikiwe.

Wachawi wanapotoka ndani ya mwili wanaangalia alama yako ya mpaka inaishia wapi. wao wana uwezo wa kupunguza mipaka ya miaka ya mtu kutoka themanini mpaka ishirini. Inawezekana wewe alama yako ya mpaka wako umepangiwa umiliki na kusafiri lakini wachawi wamesogeza mpaka wako na kuuondoa ili usifike pale unapotakiwa kufika umiliki. Unaweza ukawa alama yako ya mpaka imesogezwa na magonjwa yameanza kukupata fahamu kwamba alama yako imesogezwa ili ufe kabla hujatimiza yale uliyopangiwa.

Lazima umiliki yale unayotakiwa kumiliki na alama yako ya mpaka iliyosogezwa lazima upanuliwe kwa jina la Yesu. Unaweza ukawa una ugonjwa wa moyo ili ufe au una ugonjwa wa kisukari ili ufe fahamu kwamba alama yako ya mpaka imesogezwa hivyo basi na wewe unatakiwa uingie kwenye ulimwengu wa rohoni useme “katika jina la Yesu Kristo ninaondoa alama ya mpaka wa magonjwa ili nife kwa jina la Yesu kristo”. 

Wanasogeza ili pale unapotakiwa kufika usifike. Shetani anaweza akawa ameandaa vikwazo kwenye alama yako lakini Mungu anaondoa vikwazo vyote na kukuongezea mpaka wako kwa jina la Yesu.

Leo siku ambayo Yesu amefufuka tunaongeza alama ya mpaka yetu ili tuwe imara na kutimiza makusudi tuliyopewa na Mungu kwa damu ya Mawana Kondoo Yesu

Ukiri:
“Watu wote kwenye familia yangu ambao hawanipendi kuanzia leo ninaondoa mipaka waliyoniwekea kwa damu ya Yesu, ninapanua mipaka yangu kwa jina la Yesu na lile shimo walilochimba naamuru watumbukie wenyewe na lile jiwe waliloniviringishia litawaponda wenyewe kwa jina la Yesu, kwa jina la Yesu aliyepunguza mpaka wangu wa kuishi maisha marefu ili nife kabla ya wakati wangu ninamrudishia yeye mwenyewe kwa jina la Yesu”

Kuna mapepo ambayo hufanya kazi ya kuua wakiwa nje ya mtu au ndani ya mtu.

Zakaria 3: 1 “Kisha akanionyesha Yoshua, kuhani mkuu, amesimama mbele ya malaika wa Bwana, na Shetani amesimama mkono wake wa kuume ili kushindana naye.“

Matendo ya mitume 16:16 
Inawezekana alama yako inasimamiwa na mizimu ya familia, wanadamu wachawi, majoka, mganga wa kienyeji haijalishi ni nani amesimamia alama yako na kuipunguza, hizo zitangoka kwa jina la Yesu, 

Alama za mauti nazingoa kwa jina la Yesu Kristo . Maana ya mauti ya Yesu msalabani ni kwamba, Mungu alipoangalia duniani aliona wote tunasthili kufa lakini akaona ni vyema amtume mwanaye wa pekee ilia je atununue kwa damu yake, Yesu alikuja duniani li kufanyika kafara kwaajili ya kungoa alama zilizosogezwa na mawakala wa shetani zirudishwe mahala pake kwa Damu ya Yesu.

Source: Gospel Kitaa

Comments