RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

UNATAKA KUSAIDIAWA WAKATI HUNA UMOJA NA WENZAKO-UNAHITAJI MTU WA NNE

Siku ya Jumapili 10.04.2016, Mch Noah Lukumay wa kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni “B” kwa aliweza kusiitiza juu ya Umoja katika somo lake la “Kukutana na Mtu wa Nne”, alisema, Naomba tusome MWANZO 11;1-6. Nchi yote ilikuwa na lugha moja na usemi mmoja. Ikawa watu waliposafiri pande za Mashariki waliona nchi tambarare katika nchi ya Shinari, wakakaa huko. Wakaambiana haya na tufanye matofali badala yam awe, na lami badala ya chokaa. Wakasema haya na tujijengee Mji na Mnara na kilele chake kifike Mbinguni, tujifanyie jina ili tusipate kutawanyika usoni pa nchi yote. BWANA akashuka ili auone Mji na Mnara waliokuwa wakiujenga wanadamu. BWANA akasema tazama watu hawa ni Taifa moja, na lugha yao ni moja, na haya ndiyo wanayoanza kuyafanya, wala sasa hawatazuiliwa neno watakalokusudia kulifanya. 


Mch. Noah Lukumay

MUNGU aliposhuka ili kuuangalia Mnara wa Babeli MUNGU aliangalia akasema ‘’Jamani eeh hawa watu wana lugha moja akisema “kufuli” na kufuli inakuja, akisema funguo na funguo inakuja. Sasa lazima tushuke tukawatawanye, walipotawanywa kila kitu kikafeli. Miujiza inashindikana kwa sababu wako watu wanakutawanya, wakishakuona umeng’ang’ana mahali pamoja wanajua huyu atapata gari au mafanikio, wanaanza kukudanganya na kusema hebu tumuambie ajaribu kwenda kanisa linguine, bila kujua unafuata, kumbe hujui kuwa unapoteza muujiza wako. Unatakiwa kujua kuwa uko kwenye foleni wakati wako wa kuitwa umefika haupo ulipo yaani kanisani kwako kwahiyo tulia kanisani kwako upate muujiza wako. Unajikuta unaanza kujilaamu mwenyewe na kusema “Mbona ninachelewa kupata muujiza wangu”, kumbe shida siyo MUNGU anayejibu au kukucheleweshea muujiza wako bali ni wewe hautaki kukaa kwenye foleni, hautaki kukaa kwenye utaratibu, unataka kujipeleka kama wewe. 

Leo nawakwaza watu lakini dose inaingia. Naomba sasa tuseme kwa pamoja, “Kuanzia sasa nitatembea na kanisa langu, nitatembea na mtumishi wangu, nitatembea na MUNGU wangu katika maisha yangu.”

Wewe usipotembelewa tu unazira na unaanza kusema “Hawanipendi kwasababu sijulikani”. Nikuulize swali, “Wewe unataka kujulikana na nani?”, Unataka watu waje wakufate nyumbani kwako wakati wewe mwenyewe huwafuati watu, huna muda na watu ukitoka tu na gari lako shah…. unaondoka, wewe unahitaji kupendwa lakini wewe hupendi watu, unahitaji kusaidiwa lakini wewe hausaidii watu, apandacho mtu ndicho atakachovuna, ukipanda ngano lazima uvune ngano huwezi ukavuna maharagwe, hakikisha unaji-connect na madhabahu lazima nayo ita- reflect ni kama kioo utakaposimama mbele yake ni lazima kikuoneshe wewe ni nani? Kwa Jina la Yesu kuanzia sasa ninaenda kutembea kwa umoja, 

ZABURI 133;1-3 Tazama jinsi ilivyo vema , na kupendeza ndugu wakae pamoja kwa umoja. Ni kama mafuta mazuri kichwani yashukavyo ndevuni, ndevu za Haruni, yashukavyo mpaka upindo wa mavazi yake, kama umande wa Hermoni ushukao milimani pa Sayuni. Maana ndiko BWANA alikoamuru Baraka. Naam uzima hata milele, 

Usikose Ibada ya Jumapili saa 3 asubuhi

Comments