MelK Premium Suits

TANGAZO MUHIMU

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BISHOP DR. M.E. ADMIN

BISHOP DR. M.E. ADMIN

SANDLANDS HOTEL KARIAKOO

USIKOSE IBADA YA KUFUNGULIWA NI SIKU TATU ZA KUFUNGA NA KUOMBA NDANI YA KANISA LA MLIMA WA MOTO MIKOCHENI B

(Picha zimepigwa na Rumafrica katika ibada ya Mlima wa Moto Mikocheni "B" Jumapili 10.04.2016)

Kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B"- Dar es Salaam, linakualika katika ibada ya kufunga na kuomba ya siku tatu kuanzia Jumatano 20 hadi Ijumaa 22/04/2016 kuanzia saa 9 mchana itakayofanyika katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" kwa Bishop Dr. Gertrude Rwakatare. Ibada hii ni ibada ya KUFUNGULIWA kwako ikiwa ni mwendelezo wa ibada iliyofanyika wiki iliyopita.

Bishop Dr. Gertrude Rwakatare

Katika kufunga na kuomba kwa wiki iliyopita watu wameweza kufunguliwa katika vifungo vya Audi shetani na sasa wanafurahia wokovu wao. Kuna watu walifungwa katika ndoa zao, masomo yao, biashara yao, ndoa zao, wengine wamekataliwa na ndugu zao ana marafiki zao, laana, mikosi, uchumba kuvunjika, magonjwa sugu, kukosa ada, kukosa kodi ya kulipa nyumba au ofisi, kudhurumuliwa, kuonewa, kusingiziwa kesi, na mengine kama hayo. Mungu aliweza kuwaokoka na hayo mateso na sasa hakika wanasema yupo Mungu wa Mlima wa Moto.


Mch. Noah Lukumay

Inawezekana wewe bado unasumbuliwa na hayo mateso hapo juu na unahitaji kujikwamua katika hayo mateso lakini shetani kakugandamiza kwenye matope umenasa unashindwa wakukunasua, lakini leo tunasema yupo Mungu anaeweza kukuokoa na hayo mateso. Kwa siku hizi tatu za kufunga na kuomba katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B", Mungu atakwenda kufuta machozi yako ya muda mrefu. Njoo ukiamini na kutarajia kupokea muujiza wako. Acha kulia peke yako wakati Mungu kawaweka watumishi wake hapa duniani watakaokuombea na wewe ukapona na hilo jaribu lako.

Bishop Dr. Gertrude Rwakatare na jopo la watumishi wa Mungu kama Mch. Noah Lukumay, Mch. Francis Machichi, Mch. Elizabeth, Mch Otieno na wengine wengi watakuwepo kukuombea na kukutamkia baraka katika maisha yako.


Hawa ni watumishi wa Mungu ambao wametengwa kwa kazi maalumu ya kuwasaidia watu na kuhakikisha wanafika mbinguni, kwahiyo usijihurumie bali fanya uwezalo kuhakikisha kwa siku hizi tatu unakuwepo nyumbani mwa Bwana. Mungu wangu akubariki na akusaidie kufika katika nyumba ya Bwana siku hizi tatu Jumatano, Alhamisi, na Ijumaa kuanzia saa 9 mchana na kuendelea. Nakushukuru kwa kunielewa na kutii ujumbe huu, Mungu akubariki sana…Amen..! Bishop Dr. Gertrude Rwakatare akiombea akina dada wenye uhitaji wa kuolewa
 Katibu wa kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B", Mzee Kibona

Mama aliyepata uponyaji wa mguu wake. Madaktari walimwambia mguu wake ni wa kukatwa
 Mama apona kidonda kilichokuwa kikitoa usaha, baada ya kuombewa Jumapili ya 10.04.2016


 Maombezi ya kufunguliwa

0