RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

VIDEO: RAIS MAGUFULI ALIVYOTANGAZA KUTENGUA UKUU WA MKOA WA ANNE KILANGO SHINYANGA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli April 11 2016 ametengua uteuzi wa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Anne Kilango Malecela na katibu tawala wa mkoa huo Abdul Rashid Dachi baada ya mkoa huo kutoa taarifa zisizo sahihi kuwa hauna Watumishi hewa.
Rais Magufuli ameeleza kuwa baada ya kupata taarifa kuwa Mkoa wa Shinyanga hauna watumishi hewa, aliamua kutuma timu ya ukaguzi iliyokwenda kufanya uchunguzi ambapo hadi kufikia jana Aprili, 10 2016 imebaini kuwepo watumishi hewa 45 huku zoezi likiwa linaendelea katika wilaya mbili za Ushetu na Shinyanga Vijijini.
>>>’Na wale wote wa Shinyanga ambao walisemekana ni zero, hakuna mtumishi hewa, walikuwa tayari wameshalipwa shilingi milioni 339.9, nimejiuliza sana, na nikajiuliza sana na kwa kweli nimejiuliza sana na kwa masikitiko makubwa, kwa nini Mkuu wa Mkoa alisema hakuna mtumishi hewa?’-Rais Magufuli

Comments