MelK Premium Suits

TANGAZO MUHIMU

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BISHOP DR. M.E. ADMIN

BISHOP DR. M.E. ADMIN

SANDLANDS HOTEL KARIAKOO

VIJANA EAGT JIMBO LA TEMEKE WAKUTANA

Vijana wa kanisa la EAGT Jimbo la Temeke wamekuwa na wakati mzuri siku ya Jumanne ya April 26 katika sikukuu ya Muungano ambapo kwa upande wao wameitumia siku hiyo kwa kufanya semina ya siku moja kufundishana neno la Mungu, jinsi gani anatakiwa kuwa kijana mcha Mungu
Sehemu ya vijana

Vijana wa kanisa la EAGT wanajulikana kama CGM kirefu chake ni Christ Gospel Messengers ( wajumbe wa Kristo wa injili) Vijana hawa wa jimbo la Temeke walikutana katika kanisa la EAGT Banana.
Walipata nafasi ya kufundishwa masomo mbalimbali kutoka kwa Muhubiri na Mwalimu George Banaly (GB) somo la Kijana na Maono. Pia Katibu mkuu wa vijana kitaifa wa kanisa hilo Mchungaji Kornerio akafundisha somo la Uinjilisti na Ushuhuduaji.
Muhubiri na mwalimu GB anasema kuwa yeye ni mzee kichwani kijana mdomoni
katibu wa vijana EAGT taifa mchungaji Kornerio

Zifuatazo ni baadhi ya picha za matukio katika
Viongozi wa vijana

Mtunza fedha wa vijana Jimbo la Temeke
Katibu ya vijana jimbo la Temeke Bwana Ambakisye Friday (kushoto) akiwa na pacha wake Bwana Ambokile
Dada mjasiriamali akiwaeleza vijana jambo


EMMANUEL MBASHA AKIIMBA

Mkurugenzi wa vijana Jimbo la TemekeVIJANA WAKAPATA CHAKULA CHA PAMOJA


SAFARI YA KURUDI MAJUMBANI IKAANZA

Aidha Katibu wa CGM jimbo la Temeke Bwana Ambakisye Friday amesema kwa sasa wanajipanga kwa ajili ya kambi ya vijana wa jimbo hilo, ambayo inatarajia kufanyika kuanzia tarehe 27 Juni hadi 1 July kwenye kanisa la EAGT City Center.
0