MelK Premium Suits

TANGAZO MUHIMU

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BISHOP DR. M.E. ADMIN

BISHOP DR. M.E. ADMIN

SANDLANDS HOTEL KARIAKOO

WATU WAFUNGULIWA KATIKA MATESO SIKU YA JUMAPILI 24.04.2016 MLIMA WA MOTO MIKOCHENI "B" JIJINI DAR ES SALAA

Hakika Mungu ni mwema, tunamuona akifanya kazi katika huduma ya Mlima wa Moto Mikocheni "B" jijini Dar es Salaam. Mungu anawafungua watu kutoka vifungo walivyofungwa kwa muda mrefu na kuwaweka huru kwa kupitia watumishi wake. Tuna kila sababu ya kumshukuru Mungu kwa matendo makuu. 

Watu wamekuwa wakimiminika katika kanisa hili kwa maombezi na Mungu amekuwa mwaminifu na ameweza kuwaponya walio wengi. 

Siku ya Jumapili 24.04.2016 watu wengi sana waliweza kufunguliwa katika mateso yao wakati wa maombezi na uponyaji. Watumishi wa Mungu waliweza kuwaombea na kuwatamkia baraka waumini wa kanisa hilo. 

Tumeona Mungu akiwafungua watu wenye mapepo, majini, waliologwa, waliofungua milango ya mafanikio, wenye shida za ndoa, walioonewa, waliolaaniwa, walitupiwa vitu vibaya, wenye majini ya mahaba, wanaoota ndoto mbaya, wenye magonjwa sugu, wenye kuhitaji kazi, wenye kuhitaji mafanikio, waliofungiwa kusoma Neno la Mungu, waolala kanisani wakati wa ibada ikiendelea ilimwasipate kujua ukweli kupitia Neno la Mungu kutoka kwa watumishi wake na shida mbalimabali.

Wewe ambaye hukufika, ibada zetu za Jumapili zinaanza saa 3 asubuhi na safiri ni bure kuanzia katika kituo cha mabasi cha Makumbusho jijini Dar es Salaam au Mwenge mataa, utaona magari ya Mlima wa Moto Mikocheni "B" wewe ingia humo.

Tembelea

KIPINDI CHA MCH. NOAH LUKUMAY KUMUOMBEA MTU MMOJA MMOJA


 `Mch. Noah Lukumay akimuombea dada anayesumbuliwa na jini mahaba
 Dada akihangaishwa na tumbo
 Huyu ni dada ambaye alikuwa akiongea kama kichaa au mtu asiyejielewa akiseam, "Sawa tunatoka" akirudiarudia wakati mwinjilisti akikemea pepo juu yakeMch. Samweli Hillary akikemea mapepo

0