RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

ALIYEKUWA MCHAWI MWENYE MAJINI 25 SAFI NYEULA (MWAROBAINI) MKAZI WA GEZAULOLE NURUNI KIGAMBONI AACHANA NA UCHAWI NA KUOKOKA

Bwana apewe sifa. Habari njema kutoka kanisa jipya la Mlima wa Moto Gezaulole Nuruni Kigamboni. Kama kanisa mmekuwa mkijitoa sana katika upanuzi wa kanisa letu la Gezaulole Kigamboni, nami napenda kuwashukuru sana na najitahidi kuleta matunda yanayotokea katika kanisa letu jipya kwa msaada wa Mungu. Watu wanazidi kuokoka na kuacha uchawi na uganga. Mpaka sasa kanisa limeshasimama na sasa wanahangaikia nzege.
 
Kutoka kushoto ni Bishop Dr. Gertrude Rwakatare, Safi Nyeula na mhudumu wa kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B"

Na leo tumemuleta Safi Nyeula ambaye alikuwa mchawi wa kutisha Kigamboni. Ngoja usome ushuhuda wake:-

Baada ya hapo mama Safi alikuwa na haya ya kusema, “Bwana Yesu asifiwe, kwa jina ninaitwa Safi Nyeula, kwetu ni Musoma lakini mimi ni mtu wa bara. Kwa jina lingine ninaitwa Mwarobaini, hili ni jina gumu sana. Mimi ni mtoto mdogo sana lakini matendo yangu yalikuwa ni makubwa. Nilikuwa na majini 25, nilikuwa na makuu upande wa baba yangu na upande wa mama yangu na mengine, nilikuwa na vitambaa vyote (chekundu, cheupe na cheusi). 
Kitambaa cheusi nilikuwa navaa upande wa mamimi (yakipanda mashetani naongea cha kwetu, akipanda kisimba navaa kitambaa chekundu, akipanda Shariff navaa kitambaa cheupe na akipanda maimuna navaa cheusi ), Nikitaka chochote nilikuwa navaa vitambaa hivyo na ninapandisha mashetani na ninaongea. Kama unashida yoyote ninakuambia na ninakutibu, kama akina mama wanahitaji wapenzi, wanaohitaji biashara, mume asimnyayase mimi nilikuwa natibu. Nilikuwa na uwezo wa kujaza samaki kwenye mitubwi ya wavuvi hasa waziwa. 
Mwaka 2002 nilianza kuugua, na nikaenda makanisa mengi bia kupata uponyaji. Walikuja wachungaji kutoka Arusha wakitaka niokoke lakini nilikataa nikawaambia ukifika wakati nitaokoka. Nilikuwa naumwa majini, na nikianza kuugua, miguu (magotini), tumbo, kifua, kichwa vinauma sana mpaka inafika point nasema, ni heri nife. 
Nilikuwa natumia pesa nyingi kwa madaktari lakini sipati uponyaji (kweli daktari hajigangi). Mimi nilikuwa ni mlevi sana, nakunywa pombe kuanzia asubuhi hadi jioni na silewi kamwe, ninaweza nikafululiza siku tatu ninakunywa pombe. 
Nikinywa hiyo pombe nilikuwa simuogopi mtu yeyote yule. Nilikuwa napiga watu na nikikupiga lazima utoke damu na ilikuwa haiwezekani nikakupiga usitokwe na damu. Na nimebahatika kuwa na mume wangu na watoto watatu. 
Lakini sasa ninamshukuru Mungu kwa kutuletea Bishop Dr. Gertrude Rwakatare Gezaulole Kigamboni ambaye amekuja kutuokoa na mkuu wetu wa majini alikuwa Kasimu Suleiman. Ndugu zangu walikuwa wanasema hawadhani kama ninaweza kusimama kwenye wokovu, lakini sasa kwa nguvu aliyonayo mama Gertrude Rwakatare nimesimama. 
Siku ya tatu ya  semina ya ufunguzi wa kanisa jipya la Gezaulole nilimuomba kaka yangu twende naye na vitu vyangu vya uchawi nikavisalimishe kwa Yesu. Nilipofika pale nikachoma vitambaa vyote na maajini yote kama jini sharifu, jini makata, jini maimuna, jini masai, jini bubu. Jini Masai likija lazima uvae kimasai. 
Nichotaka kuwambia ndugu zangu kuwa mmkiri huyu Yesu Kristo, na inabidi msikae nayo mizigo ndani na mkikaa nayo mnazidi kudidimia, mtatoka kanisa lakini bado nyumbani mna msalaba ule ule. Mungu awabariki sana

Facebook: Mountainoffire Tanzania