MelK Premium Suits

TANGAZO MUHIMU

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BISHOP DR. M.E. ADMIN

BISHOP DR. M.E. ADMIN

SANDLANDS HOTEL KARIAKOO

ASKOFU MKUU WA KANISA LA EAGT AZAWADIWA GARI
Kanisa la Evangelistic Assemblies of God Tanzania (EAGT) kanda ya mashariki kusini limemzawadia gari Askofu mkuu wa kanisa hilo Dakta Brown Mwakipesile, baada ya kushiriki ibada maalumu na makanisa ya kanda hiyo jumapili iliyopita katika ukumbi wa PTA viwanja vya sababa jijini Dar es salaam.

Viongozi na washirika wa makanisa ya majimbo matatu ya kanda hiyo ya pwani Temeke na kinondoni, walikusanyika katika ukumbi huo na kukutana na kiongozi huyo aliyewatembelea kwa mara ya kwanza tangu arithi kiti cha Uaskofu mkuu kutoka Dakta Moses Kulola, aliyekuwa Askofu mkuu wa kanisa hilo. Dakta Kulola alifariki dunia Agusti 29 mwaka 2013

Pamoja na kushukuru kwa kupewa zawadi ya gari aina ya Nissan Extray yenye thamani ya shilingi 13,000,000 ikiwa ni surprise kwake, alisema suala la kuhubiri injiri ndilo swala la msingi sana kama siri ya ushindi inayoweza kumfikisha tu mbinguni.Alisema kazi iliyo mbele ni kubwa na inahitaji kufanyika kwa kulingana na idadi ya watu inavyoongezeka kila kukicha.

Alisema kuwa watu ni lazima makanisa yaliyopo yazae na kuongezeka idadi ili kuvutia watu wengi iwezekanavyo kwa Yesu Kristo, ambapo alitoa takwimu jinsi kanisa la EAGT lilivyoanza likiwa na washirika wachache na sasa lina maelfu ya washirika.Askofu Dakta Mwakipesile alihimiza suala la utakatifu ndani ya kanisa ililiwe na nguvu ya Kimungu inayowza kulta mabadiliko.

Alisema kwa kawaida kanisa lenye nguvu ya Kimungu huweza kuzaa wakristo safi wenye nguvu hizo na ndiyo sababu ya kanisa kuwepo ulimwenguni kama ilivyokuwa kanisa ka kwanza.Aidha aliitaka kujiendesha lenyewe kwa kuitegemea kupitia utoaji na hivyo kuwa na majengo ya makanisa yatakayo wawezesha washirika kuwa huru wakati wa ibada.

Askofu Dakta Mwakipesile aliwataka washirika na viongozi wa kanisa la EAGT kuiombea selikali pamoja na rais Dakta John Magufuli, ili afanye kazi yake kwa utulivu akiwa na amani na ulinzi wa Mungu. “Sasa ni wakati wa kumuunga mkono Rais Magufuli ili kuhakikisha kuwa na amani na pia kukua kiuchumi”, alisema Dakta Mwakipesile.Askofu Dakta Mwakipesile aliendesha maombi ya ujazo wa Roho mtakatifui na watu wengi kufurika Roho huyo kwa namna ya kipekee.

Askofu Mkuu wa EAGT kulia Dr Mwakipesile akiteta jambo na waziri Mkuu Dr Majaliwa

Katika mahojiaono na Mwandishi Askofu wa kanda ya mashariki kusini wa kanisa la EAGT Nicolaus Nyenye alisema ana mshukuru Mungu kwa viongozi na washirika wa kanisa hilo kuitikia wito wakujumuika na Askofu Mwakipesile, kwa vile inaonyesha kuwa wanamtambua kiongozi wao huyo; jambo ambalo ni Baraka kwa vile amewekwa na Mungu.Naye katibu wa kanda ya mashariki kusini wa kanisa la EAGT Dakta Alphonce wanjala alisema kuwa kitendo cha kutembelewa na Askofu mkuu Dakta Mwakipesile ni kizuri kwa vile ziara hizo zinaliunganisha kanisa hilo ambalo lina kanda tisa.

Alisema kanisa la EAGT linaguswa na kubarikiwa na sera za Askofu Mwakipesile za kusisitiza utakatifu katika kanisa na suala zima la kuhubiri injili, ili kuwafanya mataifa yote wawe wanafunzi wa Yesu, kama Yesu mwenyewe alivyoagiza kwenye Mathayo 28:19.Naye Askofu wa jimbo la EAGT Temeke Florian Katunzi, kama walivyoeleza viongozi wenzake, alisema kimsingi jimbo la Temeke analoliongoza ndilo lilikua mwenyeji wa ujio wa Askofu Dakta Mwakipesile hivyo ni jambo la kumshukuru Mungu.

Alisema Dakta Mwakipesile kila mara husisitiza juu ya kukaa kwenye msingi wa neno la Mungu kwa kuzingatia imani ya kikristo sambamba na kazi ya kuhubiri injili, ambayo ndiyo uti wamgongo wa kanisa la EAGT tangu enzi za Askofu Mkuu wa kwanza wa kanisa la hilo hayati Dakta Kulola

Source:Msemakweli