MelK Premium Suits

TANGAZO MUHIMU

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BISHOP DR. M.E. ADMIN

BISHOP DR. M.E. ADMIN

SANDLANDS HOTEL KARIAKOO

BARAKA YA NDOA YAZIDI KUONDOKA NA WAIMBAJI WA KWETU PAZURI RWANDA


Moja kati ya baraka ambazo kundi la Ambassadors of Christ ya Rwanda limebarikiwa nayo ni kuona waimbaji wake wakike kupata wenzi wao wa maisha na kuanza maisha ya ndoa, hata hivyo licha ya baraka hizo njema kwaya hiyo imeonekana kupoteza waimbaji hao kutokana na majukumu ya kifamilia.


Nyota wa Kwetu pazuri Yvonne akiwa na binti yake.


Kati ya waimbaji ambao hawaonekani mara kwa mara na kwaya hiyo ni pamoja na malkia wa kwetu pazuri mwanadada Yvonne tangu amepata binti yake wa kwanza kuonekana kwenye kwaya kumekuwa kwakusuasua, Kelly Ndaga naye pia tangu afunge ndoa hajawahi kuonekana kwenye DVD mpya za kwaya hiyo, huku mwanadada mwingine mkongwe Patience Pepe aliyeolewa na mzungu raia wa Australia bwana James Webb, ameondoka na mumewe huyo kuelekea Australia hivi karibuni.

Hata hivyo licha ya mapengo ya wakongwe hao ambao bado wanatarajiwa kujiunga tena watakapopata nafasi, kwaya hiyo imeonekana kutokuyumba kutokana na kasumba ya mwalimu wa kwaya hiyo bwana Sozzi kuwa na utaratibu wa kuwafundisha wanakwaya wake wote kujitegemea kwenye suala la uimbaji na kusolo nyimbo.

Katika picha hii wadada wote wameolewa isipokuwa Sarah aliyesimama na Yvonne, ambapo kati yao ni waimbaji wawili tu wakike waliobaki mpaka sasa.

Ambassadors of Christ ndio kwaya ya kwanza Afrika (kwa uchunguzi wetu GK) kurekodi album zake kwa kutafsiri katika lugha mbalimbali na kuwaletea mafanikio makubwa. Kway nyingine ambayo imewahi kufanya hivyo ni kwaya kongwe ya Holy Cross ya Afrika ya kusini ambao walikuwa wakitafsiri nyimbo zao kwa lugha ya kabila lingine huko Botswana

Source: Gospel Kitaa