TANGAZO MUHIMU

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BISHOP DR. M.E. ADMIN

BISHOP DR. M.E. ADMIN

SANDLANDS HOTEL KARIAKOO

BISHOP DR. GERTRUDE RWAKATARE: SUMAKU YA KIROHO YA KUNASA VITU VIILIVYONASA KATIKA MAISHA YETU HAVIENDI MBELE


Bishop Dr. Gertrude Rwakatare katika ibada ya Jumapili 01.05.2016 Mlima wa Moto Mikocheni “B” alifundisha mambo mengi lakini leo na kupa kipengele hiki cha uwezo wa sukumaku kuvuta vitu vilivyonasa, alisema, “Afya yako ambayo ni mgogoro leo nahamisha hapo. Muone Askofu wetu Dkt. Gertrude Rwakatare uzee wake hauonekani kanisani kutokana na jinsi Mungu anavyombariki na kusababisha kuonekana kijana; sasa kwa upako wa Kiaskofu pokea muujiza wako, pokea kuinuliwa kwa Jina la Yesu. Maandiko yanasema, 
Bishop Dr. Gertrude Rwakatare

’Ile miaka iliyoliwa na badu badu, iliyoliwa na balale, iliyoliwa na wachawi, leo ni lazima irejeshwe kwa Jina la Yesu. Waliokuchukulia fedha ni lazima wairejeshe, “double double”, walioichukua haki yako ni lazima irudishwe, hakuna kitu kitapotea. Tatizo la watu wengi huwa wanaenda peke yao huko wanakoenda na wakinasa ndio utawasikia, ‘’Mchungaji upo? natakakuja’’ 
Sasa mbona ulivyokuwa unaenda hata hukumshirikisha? Maandiko yanasema mwanafunzi humshirikisha mkufunzi wake katika mema na mabaya’’ Kila unapotaka kufanya jambo mshirikishi mtumishi wako ili mambo yakiwa magumu akusaidie. Kuna mtu aliazima shoka na alipotaka kutumia likadondoka shimoni, na akaanza kujiuliza ‘’Ni kwanini nilichukua shoka la kuazima? 

Kwanini niliazima? Lakini akamuendea Mtumishi akamwambia shoka ni la kuazima, siyo langu la mkopo. Sasa inawezekana mkopo wako umegoma kwenye tiba, kwenda China kufunga mali, vyanzo vya fedha, ghorofa ambalo halijaisha. Ukiona hivyo unaanza kusema, “Mtumishi wa MUNGU mkopo wenyewe siyo wa kawaida bali ni wa hatari, nitauzwa na watoto wangu lakini bado hatutalipa, Mtumishi wa MUNGU tusaidie wewe una uwezo wa kutoa shoka lililoingia shimoni, mtumishi wa MUNGU akamwambia imeangukia wapi, unajua huwa tunaulizia kama vile ni masihara, 
akamwambia imeangukia hapa, akiangalia chuma imezama chini lakini mtumishi wa MUNGU akachukua kijiti akakirushia pale lakini ile chuma ni nzito lakini sumaku iliyokamata ilikuwa ni ya Mtumishi wa MUNGU. 
Leo napeleka sumaku ikakamate iliyokuwa ni haki yako, leo napeleka sumaku ikavute nyota yako, ikachukue biashara yako. sumaku ni kitu kingine hata kama hakionekani na inadhauriwa. Sasa,watoto wamegoma na wako tumboni lakini sumaku itavuta watoto wako. 
Ulikuwa hupati watoto lakini sumaku itavuta watoto wako ikaingia kwenye tumbo lako, wewe huwezi ukaona lakini sumaku inaweza ikaleta miujiza, wewe huwezi ukaona lakini unaweza ukavutiwa kile kilichopotea, nakutangazia kwamba yale mambo ambayo watu wamepoteza leo virudi kwa Jina la Yesu, kuna watu wanakupeleka nje ya mji leo tunakurudisha, wanataka usiolewe leo tunakutangaza ndoa yako kwa Jina la Yesu