RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BISHOP GERTRUDE RWAKATARE ASHTUA MIOYO YA WATU KWA MAFUNDISHO YAKE YA JUMAPILI 22.05.2016 MLIMA WA MOTO MIKOCHENI "B"

HAKUNA WA KUJITETEA KUWA HAJAMUONA MUNGU
Bishop Dr. Gertrude Rwakatare siku ya Jumapili 22.05.2016 aliweza kuhubiri mengi na baadhi ya mahubiri yake ni kama haya, alisema, “Bwana Yesu asifiwe, Tusome Waebrania 2:3-4. Hapo mwanzo Manabii walitokea na kusema amezaliwa Yesu mkombozi wa ulimwengu, na Yesu mwenyewe akatuthibitishia, na Yesu mwenyewe tumemuona akiokoa, na zaidi ya hao tumeona wenyewe kwa macho yetu miujiza, ishara na maajubu ndani ya wokovu. 
Hakuna atakaye jitetea kuwa sijamuona Mungu. Tumemuona Mungu kwa njia moja au nyingine, wapo waliokuwa chini na Mungu akawainua wakawa juu, wagonjwa Mungu akawaponya, wako waliokuwa na shida ya kupata watoto na Mungu amewapa watoto. Mungu alitenda muujiza kwa waliokuwa na umri mkubwa Mungu akawapa waume, watu tumeona kwa macho yetu miujiza, watu waliofungwa na majini mahaba wakikombolewa. Nakuomba uzidi kuishi maisha ya imani ili siku moja tukakutane mbinguni kwa Baba.


WATU WAMEDHARAU WOKOVU
Jamani tutapate kupona tusipojali wokovu mkuu namna hii.. Watu wamedharau wokovu, wamepuuzia, wamekaa wamekomaa, wamefanya Mungu ni babu wao, watu wamemzoea Mungu na wanamuona kana kisamvu kilichochokaa.

Kila siku fanya wokovu mpya. Uliokoka endelea kuokoka ili tutakutane mbinguni. Ishi maisha Matakatifu, ishi maisha ya kumpendeza Mungu, kila siku uwe na hofu ya Mungu, nenda kahubiri Injili mbele za BWANA ili watu waokoke. Tusiwe kama Esau alipokuwa na njaa alimwambia mdogo wake niuzie uzao wako wa kwanza nitakupa dengu.
Kila siku ungama upya, kila siku sali upya, kila siku anza upya. Uwe Mtakatifu kama Yeye (Mungu) alivyomtakatifu. Mungu akusaidie uyatii haya niliyokushauri ili siku moja tukamuone Mungu

HUJUI LITAKALO KUKUMBA DAKIKI MOJA ILIYOMBELE YAKO
Kuna Dada mmoja mwinjilisti ambaye alijilinda sana vizuri na mambo ya uasherati kwa muda mrefu. Siku ya graduation yake, watu wakafanya sherehe, wakacheza wakafurahi. Ulipofika usiku wa manane dada huyo akashindwa kwenda nyumbani peke yake. 
Kulikuwepo na jamaa moja alikuwa akimuwinda kwa muda mrefu akitaka kufanya naye mapenzi, akamwambia sasa twende nyumbani kwangu ukalale, ingia kwenye gari yangu. Dada huyo akasema hakuna shida akaingia kwenye gari ya huyo kaka mpka nyumbani. Walipofika nyumbani kwa huyo kaka, akamwambia siku zote nilikuwa nakutaka unalinga na leo umeiongia laini, umeingia kwenye 18 zangu, sasa unasemaje kuhusu kufanya mapenzi?. 
Dada akaanza kukataa, yule jamaa akamlazimisha mpaka dada huyoakaingia laini akakubali kufanya naye mapenzi. Dada yule akajiambia katika nafsi yake kuwa atatubu kwa Mungu, atafunga na kuomba. Asubuhi ilipofika yule dada akachukua tax, na alipofika mbele kidogo tax ikapata ajali, akafa yeye na dereva hakufa.


HUJUI LITAKALO KUKUMBA DAKIKI MOJA ILIYOMBELE YAKO. TUBU SASA
Dada mmoja mwinjilisti ambaye alijilinda sana vizuri na mambo ya uasherati kwa muda mrefu. Siku ya graduation yake, watu wakafanya sherehe, wakacheza wakafurahi. Ulipofika usiku wa manane dada huyo akashindwa kwenda nyumbani peke yake. 
Kulikuwepo na jamaa moja alikuwa akimuwinda kwa muda mrefu akitaka kufanya naye mapenzi, akamwambia sasa twende nyumbani kwangu ukalale, ingia kwenye gari yangu. Dada huyo akasema hakuna shida akaingia kwenye gari ya huyo kaka mpaka nyumbani. Walipofika nyumbani kwa huyo kaka, akamwambia siku zote nilikuwa nakutaka unalinga na leo umeingia laini, umeingia kwenye 18 zangu, sasa unasemaje kuhusu kufanya mapenzi?. 
Dada akaanza kukataa, yule jamaa akamlazimisha mpaka dada huyo akaingia laini akakubali kufanya naye mapenzi. Dada yule akajiambia katika nafsi yake kuwa atatubu kwa Mungu, atafunga na kuomba. Asubuhi ilipofika yule dada akachukua tax, na alipofika mbele kidogo tax ikapata ajali, akafa yeye na dereva hakufa. Unajifunza nini?

ITAKUSAIDIA NINI KUPATA VYOTE VYA DUNIA UKAKOSA MBINGU?
Hakuna maandiki yoyote, kwa kupoteza wokovu wako. Yesu alikataa, alisema mtu hataishi kwa mkate bali kwa Neno la Mungu. Na wewe unatakiwa kujiambia kila siku. 
Naomba usoma Marko 8:36, Itamsaidie nini mwanadamu kupata ulimwengu wote na baadae akaipoteza nafsi yake yote. Shikilia wokovu, ukiona sisi wazee tunaendelea na wokovu ujue kuna kitu katika wokovu.
Vya duniani vinapita, wazuri wanapita. 
Mwingine anasema “I’m too handsome” na wadada wanajigonga kwake, lakini kulikuwa na Yusufu katika Biblia ambaye alikuwa “handsome” na mke wa mfalme alimtaka, na yeye aliamua kumuachia nguo yake akakimbia zinaa. 
Dunia ni sifuri yenye masikio, kwa vijana na wazee ni ubatili. Mwanamke uliyemuacha na kusema ngoja ujaribu wa Tanga, lakini unatakiwa kujua kuwa ni wamoja, ni shetani tu, hakuna chochote, ni ubatili tu. Unajua kuna wazee wakifika middle class wanakuwa wasumbufu sana, mzee mmoja akaniambia, “Mchungaji siku hizi wanawake ni wazuri sana” Nikajua huyu amebanwa na hajui kuwa vyote ni ubatili tu. 
Aliyemweupe ni sawa na aliyemweusi, aliyemfupi nyundo ni sawa na mrefu, aliyemnene ni sawa na mwembamba. Tushike imani, tusimame na maombi yetu tuliyoungama nayo hapo mwanzo. Ninakuambia Mungu yupo na Mungu anatenda, ninakuambia mbingu iko. Ukifanya vizuri utaenda mbinguni na ukifanya vibaya utaenda motoni, na moto upo kweli. 
Wengi wanataka mahubiri wakati wa kifo, wakati wa misiba. Lakini mahubiri haya ya kila siku hawayajali kabisa, wako “busy” na dunia. Basi ninakuomba pamoja na u-busy wako lakini usitende dhambi tena, kwa maana wokovu ni kutotenda dhambi tena. Hata kama pesa zingekuwa nyingi ni ubatili, hata wakisema wanakujengea nyumba hiyo nyumba utaiacha, utakwenda uchi kama ulivyozaliwa kwahiyo mg’ang’ania Yesu Kristo. 


Tembelea


MATUKIO KATIKA PICHA