RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

FACEBOOK YAPATA FAIDA YA DOLA BILIONI 1.5



KAMPUNI ya Facebook imeripoti ongezeko la faida ya asilimia 195 katika robo ya kwanza ya mwaka huku kampuni hiyo ikiendelea kupata mapato ya matangazo mapya.

IIiripoti mapato ya dola bilioni 1.5 katika kipindi cha kati ya mwezi Januari na Machi ikilinganishwa na mapato ya dola milioni 512 mwaka uliopita.

Mbali na kuwapatia wenye matangazo huduma mpya kama vile video, Facebook iliimarisha mauzo yake kutokana na huduma zilizopo.

Facebook pia imependekeza mpango mpya wa hisa ambao utampatia fursa mwanzilishi wake Mark Zuckerberg kuuza hisa zake bila kupoteza udhibiti wa kampuni hiyo.

Kampuni hiyo imesema kwamba hatua hiyo itamtia moyo Zuckerberg kusalia katika uongozi wa Facebook.

Thamani ya hisa za Facebook ilipanda hadi asilimia tisa baada ya kufanya biashara.

CHANZO: BBC SWAHILI
30SHARES