HABARI PICHA: KINACHOJIRI JUMBA LA WASHINDI INSPIRED 4 CHANGE


Ikawa jioni na kukakucha, siku ya pili ya Inspired 4 Change ikawadia na saa ikatimia mabapo vijana wakapatiwa ufunuo kutoka kwa Mungu kupitia wanenaji wake,
Kubali kusafiri na Mungu kama kijana, nawe hutopotea. - Mch Lucy.

Aprili mwaka 2015, ndipo msimu wa kwanza wa Inspired4Change ulianza ukilenga mabadiliko kwa vijana wa kanisa. Ujasririamali na namna ya kuwekeza ndio ilikuwa mada kuu kwa tukio hili ambalo lilifanyika nje ya kanisa. Baada ya hapo, wengi wameweza kubadilika na kuchukua hatua ikiwemo kutafuta mashamba na hata mikopo kwa ajili ya kujiendeleza.
Na hatimaye msimu wa pili ndo huu ambao nao umekuwa wa kipekee, ambapo ndani ya madhabahu ya watu walioshinda (Victory Faith) ndipo mahala vijana wamekutanishwa. Huduma kadhaa zimeungana kuwezesha kufaniskisha kwa tukio hili; ikiwemo Watoto, Wababa, Wakinamama, na kanisa zima kwa ujumla wamefanikisha jambo hili, ikiwemo Machalii wa Yesu na wengine kadha wa kadha.

Zifuatazo ni picha aa kinachojiri kwa hivi sasa kutoka hapa Kijenge Mwanama, Victory Faith Jumba la Washindi.

- See more at: http://www.gospelkitaa.co.tz/2016/05/habari-picha-kinachojiri-jumba-la.html#sthash.dWMiPGk8.dpuf