RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

HUYU NDIYE BINTI WA RAIS WA CAMEROON ALIEZWA HOSPITALI KUTOKANA NA KUZIDIWA NA MATUMIZI YA MADAWA YA KULEVYA.

EXCLUSIVELY..!! Binti pekee wa Rais wa Cameroon Paul Biya anaefahamika kama Brenda Biya ameripotiwa kulazwa kwenye hospitali moja jiji Los Angeles nchini Marekani tangu May 11,akiuguzwa na Mama yake mzazi Chantal Biya ambae ni mke wa rais wa Cameroon huku chanzo cha ugojwa wake kikitajwa kuwa ni kuzidiwa na matumizi ya madawa ya kulevya.

Rais wa Cameroon Paul Biya na mkwe Chantal Biya.

Wiki iliyopita binti huyo mrembo alipost video kwenye mtandao wa Snapchat akivuta kitu kinachodaiwa kuwa ni bangi ambapo video hiyo ilipelekea raia wa taifa hilo linaloongozwa na Baba yake kuikosoa familia ya kiongozi huyo hasa jinsi binti huyo anavyotumia fedha kufanya starehe na marafiki zake kitendo kinachotafsiriwa kama dharau kwa wananchi hasa wanaoishi maisha duni.


 
 Brenda Biya.

Kwa mujibu wa mtandao wa Pulse,sio mara ya kwanza kwa binti huyo kuhusishwa na skendo za matumizi ya madawa ya kulevya kwani taarifa zinadai kuwa binti huyo amekua akipost video clips kwenye account zake za social media akivuta bangi na aina nyingine madawa ya kulevya.
Mpaka sasa hakuna taarifa rasmi kutoka kwenye familia ya kiongozi huyo ingawa inadaiwa tangu binti huyo alipolazwa video zinazomwonyesha binti huyo akismoke ganja zimefutwa kwenye account zake,japo tayari video hizo zilishasambaa na kufika kwenye maktaba za mapaparazi.