TANGAZO MUHIMU

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BISHOP DR. M.E. ADMIN

BISHOP DR. M.E. ADMIN

SANDLANDS HOTEL KARIAKOO

KUTANA NA HARAKATI ZA DANNY KIBAMBE AKIWA NCHINI UJERUMANIMwanamuziki mahili wa kundi la Glorious Worship Team (GWT) Danny Kibambe ambaye kwa sasa yuko nchini Ujerumani, ameijuza Hosanna Kwanza kuwa yupo nchini Ujerumani toka tarehe 15 March 2016 akifanya muziki na Bendi iitwayo Circus.Kabla ya kwenda ujerumani Danny alikuwa nchini Marekani kisha alirudi nchini na badaye akaelekea nchini Ujerumani aliko mpaka hivi leo.Haya ni mahojiano ya Hosanna kwanza na Danny

Hosanna kwanza:Unauonaje muziki wa Tanzania ukilinganisha na level za Germany?
Danny Kibambe:Wenzetu wako mbali lakini na sisi tunafanya vizuri kwa sehemu yetu japokuwa Muziki ni mpana sana kikubwa ni kuendelea kunyenyekea na kujifunza zaidi.

Hosanna Kwanza: Ukiwa Ujerumani una miss nini hasa kutoka Tanzania

Danny Kibambe: Duuhh Kwanza Kampani (Marafiki) nawamiss mno pia madarasa yangu ya Vocal Training, am a Vocal Trainer,pia nkiwa Bongo nlikuwa nafanya kazi part time na studio nne tofauti so namiss hivyo.

Danny akiwa na mama yake nchini Marekani mwaka 2013

Hosanna Kwanza:Nini mipango yako ya baadaye katika muziki

Danny Kibambe:Binafsi nataka muziki wangu ufike mbali na ninatarajia kufungua studio yangu binafsi pindi nkirudi bongo(Tanzania)

Hosanna Kwanza:Danny umefanya muziki muda mrefu tueleze kwa mtazamo wako kwa wapigaji wa Keyboard nchini ni nani unamkubali sana?

Danny Kibambe: Ki bongo bongo aisee namkubali Jimmy Kimutuo jamaa yuko vizuri pia najikubali mimi mwenyewe pia.

Baada ya kurudi nchini akitokea ujerumani Danny anatarajia kufanya tamasha la Kusifu na Kuabudu jijini Mwanza akishirikiana na kanisa la Hosanna Christian Centre chini ya Hosanna Praise Team.

Makala hii imeandikwa na Adolph Robert Nzwalla

Source: Hossana Kwanza