MelK Premium Suits

TANGAZO MUHIMU

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BISHOP DR. M.E. ADMIN

BISHOP DR. M.E. ADMIN

SANDLANDS HOTEL KARIAKOO

MCH. NOAH LUKUMAY: TAMBUA MUUJIZA WAKO


Siku ya Jumapili 01.05.2016 katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni “B” Noah Likumay alikuwa na haya ya kusema , Zakayo alipokuwa akipanda juu ya mbuyu watu walimshangaa kumbe alikuwa anatafuta muujiza wake, na wewe uliyoko hapa Mlima wa Moto Mikocheni “B”ni lazima upate muujiza wako, . Waliokuwa wanakudharau watakuheshimu ukiwa juu. Ni lazima urejeshewe heshima yako. Lazaro alikuwa anadharaulika na kila mtu alikuwa anamchukia anamuona mtu wa chini, lakini alipojiunganisha na network ya Mungu akakubalika.Yesu akaangalia Lazaro akasema huyu mtu siyo wa kawaida. Yaani kuna mitandao mahali fulani inayosababisha networks zikubaliane, yaani hata kama kuna mahali unafukuzwa mtambo unasababisha ukubalike kwa Jina la Yesu. Leo nakuunganisha na upako wa kibali chako, leo nakuletea upako wa kurejeshewa.


Mch. Noah Lukumay

Mama mmoja alifiwa na mtoto wake lakini akajua huyu mtoto ametoka kwa utambi, akamwambia Mtumishi wa MUNGU ,mbona umenihadaa? Yule mtoto ambaye umenipa ashakufa, alipokufa yule mtoto akaambiwa na mtumishi mmoja aapeleke fimbo akaweke juu ya mtoto, na alipopeleka ile fimbo jamaa akarudi akasema fimbo haijaleta matokeo, akapeleka tena akasema lakini bado haijaleta majibu, akambiwa irudishe lakini kabla hajairudisha mtambo (network) ukanyanyuka wenyewe. 
Leo napeleka mtambo (network) kwenye biashara yako, mambo yako ambayo yameshindikana leo naingiza mtambo (network), waliokucheka watasherehekea na wewe, waliokudharau watachekelea na wewe, waliosema haufanikiwi watasherehekea.
Akanyanyuka jamaa akaenda kwa madaha akienda taratibu, mtoto amekataa fimbo, amekataa mtu uliyemtuma sasa mimi mwenyewe nimekuja sasa, akakutana na huyu mtoto amenyamaza kimya akamwambia leo ninaingiza kilichomo ndani yangu kiingie ndani yako. Sasa kama una imani na Askofu Gertrude Rwakatare biashara yako inakwenda kunyanyuka leo, pokea kwa imani, sema amina.