MCHUNGAJI JOYCE JIMMY WA KANISA LA LIVING WATER CENTRE KUZIKWA LEO

Mchungaji Joyce Jimmy wa kanisa la Living Water Kawe Makuti tawi la Buza alifariki dunia tarehe 23/5/2015. Msiba huo umetokea Jumamosi asubuhi siku moja baada ya kujifungua kwa operation.Msiba uko Mbagala nyumbani kwake na mazishi yatafanyika leo 25/5/2016 katika makaburi ya Chang’ombe. Rumafrica na Hosanna Kwanza inawatakia Pole kanisa la Living Water Centre linaloongozwa na Apostle Onesmo Ndegi na familia nzima ya Mchungaji Joyce Jimmy.