RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

MFANYABIASHARA MASHUHURI WA MADINI CHUNYA MBEYA BWANA FADHILI AKIOMBEWA KUPONA KUVIMBA MWILI KATIKA KANISA LA MLIMA WA MOTO MIKOCHENI "B" NA BISHOP DR. GERTRUDE RWAKATARE

Mfanyabiashara mashuri wa madini Chunya Mbeya Tanzania Bwana Fadhili na familia yake (mke, dada) waliweza kufika katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" jijini Dar es Salaam siku ya Jumapili 34.04.2016 kwaajili ya kuombewa ili apone tatizo la kuvimba mwili na hasa mikono na miguu. Dada yake akiongea kwa uchungu aliliambia kanisa kuwa yeye alipopata taarifa kuwa kaka yake anaumwa sana na hawezi kwenda kusimamia biashara zake kutokana na tatizo la kuvimba mwili na hususani miguu na mikono aliamua kuchukua hatua ya kumshawishi afike kanisani kwa Bishop Dkt. Gertrude kwaajili ya maombezi. Bwana Fadhili hakuwa mwepesi wa kukubali kufika katika kanisa hilo kwasababu yeye ni Mwislam na hapo hapo alikuwa ameshapanga ratiba ya kwenda kwa waganga wa kienyeji kwajili ya matibabu. Lakini dada yake alimsisitiza sana ajitahidi kuja kanisani kwaajili ya kuombea ili apone, Fadhili alikubali na kufunga safari yake kuja Dar, na alipofika Mafinga aliamua kulala na siku ya pili akaanza safafri ya kuja Dar es Saaam. Alipofika dar aliweza kumtafuta mke wake anayeishi Mbagala na kuweza kulala pale kwaajili ya kuja kuombewa Mlima wa Moto Mikocheni "B"
Dada wa Bwana fadhili akiongea. Anayefuta kutoka kulia ni mke wake

Bishop Dr. Getrude Rwakatare (mama wa upendo) aliweza kuwaomba wachungaji wa kanisa na kanisa zima kuelekeza mikono yao kwa Bwana fadhili na kuanza kuomba. Wakati maombezi yakiendelea Bwana fadhili alisema aliona kitu kizito kinamvuta chini na kilimsababishia kudonga chini.

Baada ya maombezi kumalizika Bishop Dr. Gertrude na wachungaji waliweza kumpaka mafuta ya upako mwili mzima kwajili ya kuondoa uvimbe. Tunamshukuru Mungu bwana Fadhili aliweza kutembea na kucheza music kanisani kumshukuru Mungu kwa uponyaji wake. Tuzidi kumuombea Bwana Fadhil aweze kudumu katika wokovu wakati huu na baadae. Munguakubariki sana
 Miguu akiwa imevimba
 Wachungaji wakiomba




 Akicheza