RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

MGANGA MKUU NA MCHAWI SALUM SULEIMAN ALIYETAKA KUMDHULU BISHOP DR.GERTRUDE RWAKATARE AACHA UCHAWI NA KUOKOKA MLIMA WA MOTO GEZAULOLE-GIZANI KIGAMBONI JIJINI DAR


Kwa jina naitwa Kassim Salum Suleiman na mke wangu anaitwa Eliza Kitigwa kazi yangu ilikuwa ni mganga wa kienyeji mgangaa mkuu na mchawi mkuu wa Gezaulole-Gizani Kigamboni hapa jijini Dar es Salaam.

Kutoka kushoto ni Mch. Noah Lukumay, Bishop Dr. Gertrude Rwakatare, Kassim Suleiman na mke wake, Mch. Francis Machchi na Mch. Otieno (nyuma)

Siku moja Askofu Dkt. Gertrude Rwakatare alifungua kanisa jipya huko Gezaulole-Gizani ambayo kwa sasa hivi inaitwa Nuruni, waliweka spika zao zilizokuwa na sauti kubwa nje ya uwanja wa kanisa hilo kwaajili ya ufunguzi wa kanisa na kongaman. Mimi nikiwa kwenye ofisi yangu ya uganga nikasikia matangazo ya Injili wakisema waganga na wachawi watakufa .
Tamko hilo lilikuwa ni chukizo kwangu kwahiyo nikawa najisemea moyoni, ngoja nifike pale mahali halafu nimuone huyo Mtumishi wa MUNGU anayesema “wachawi watakufa”. Kwa msaada wa MUNGU niilifika mahal pale nikiwa na kusudi langu kwa matamshi aliyotamka Yule mtangazaji kuwa wachawi watakufa, kwahiyo nilikwenda nikiwa na pembe yangu ambayo ilikuwa ina nguvu ya majini. Nilipofika eneo la mkutano nikamuona mama Askofu Dkt. Gertrude Rwakatare akiwa amekaa jukwani akijiandaa kwenda kuhubiri Neno la MUNGU, mimi nikatoa ule upembe wangu mfukoni na nikauamrisha ili asiweze kusimama pale alipokaa, cha ajabu kilichonikuta niliunguzwa na moto mkali. Kumbuka ya kwamba kila nikiamrisha pembe yangu ya mara nyingi hufanya kazi lakini kwa Askofu ilishindwa kabisa.
Baada ya kuona hakuna kilichotokea kwa siku hiyo ya kwanza sikuridhika kwahiyo nikarudi tena siku ya pili nikaongeza tena nguvu ya uchawi cha ajabu moto ukanichoma tena na ule utembe ukawa tena haufanyi kazi, yaani remote ya kichawi ya kwanza ikawa imekufa na ya pili ikawa imekufa tena, nikasema tena hata sikubali kushindwa nilikuwa nina vioo vyangu viwili vyenye kushika masafa marefu kichawi (darubini au tv ya kichawi) ambacho hata nikiwa nyumbani kwangu na wewe uko mbalii naweza nikakuita ama nikasema njoo akakuona, nilipofika ofisini kwangu nikajiandaa vya kutosha kwa kutumia kile kioo changu cha uganga na rada iliyokuwa inakaa chini ya mlango wangu nikawa nasema namvuta Yule Askofu mama Gertrude Rwakatare na ninaamrisha yale mahubiri yaliyokuwa yanahubiriwa pale yaziweze kufanya kazi katika nguvu za giza kukata mawasiliano, 

lakini cha ajabu kile kioo changu kikagawanyika yaani kikapasuka tena, nikaendelea tena kioo cha pili nikaamrisha tena nikamvuta na kukiamrisha lakini na chenyewe pia kikaharibika na kuchanika, baada ya hapo nikaishiwa nguvu na ujanja, na mimi nilikuwa ni mganga mkuu na mchawi na nilikuwa ninamiliki majini yapatayo arobaini (40) ya kunisaidiia kazi mbali mbali, na waganga waliokuwa chini yangu ambao walikuwa wananitegemea mimi walikuwa wapatao ishirini na tano(25), wakija kupata huduma ya kusaidiwa nguvu za giza. Baada ya kuishiwa nguvu nilijiuliza sana sina ujanja tena, 

mke wangu hajui kilichotokea ilibidi nimvute mke wangu na nikamueleza hali halisi ya kile kilichotokea kule Mlima wa Moto Gezaulole-Gizani Kigamboni. Siku hio hio jioni sikuwa na kitu lakini roho ilikuwa inanituma niende tu nikakuta wanagawa vitambaa vya upako ambavyo mama Askofu Dkt. Gertrude alivileta. Imani ikaniijia kupitia maneno yao (waliokuwa wanagawa vitambaa) ya kwamba vitambaa hivi ukivipata vina baraka kwa wafanyabiashara mbali mbali, na kwa waliokuwa wana shida na matatizo mbali mbali, nami ikabidi nikichukue, nilipokichukua tu roho ikawa inaniambia niingie pale katika miongoni mwa watu waliokuwa wanaokoka ili nikaokoke.
Pia pale nilipokuwa ninakaa palikuwa na nyumba ya mizimu na majini ambapo nikichukua mikuki yangu nikiweka nje kama nikipewa kazi ya masafa marefu pengine mbali kulko Dar es salaam nikiunganisha na nikiiamrisha inakuwa ni kama mizinga inaenda masafa marefu na inamfikia mtu niliyemlenga, hiyo ndiyo kazi kubwa na mawasiliano nilikuwa nina rada moja kubwa ya kichawi niliyokuwa nimeiweka chini mlangoni kwangu niliichimbia chini ya ardhi ambayo inafanya mawasiliano na anga ya juu, chini ya ardhi, na hata hapa hewani. Yaani ile rada ilikuwa ndio mtambo wako wa kunasa mawasiliano, au ni kama mnara ambapo nikisema Mwanza inafika, Kigoma inafika. Lakini sasa hivi mimi nimeamua kuachana nayo kabisa.

Kitu cambacho ninapenda kuwaambi watu wanaoisoma hii haabari ni kwamba ninamshukuru sana huyu mama Askofu Gertrude kwa sababu ana upkako wa pekee na ni hazina kwa Tanzania nzima na duniani kwa ujumla ni mara yangu ya kwanza kuona hali hii, pilinawashukuru sana Wachungaji waliopewa upako na mama Gertrude Rwakatare wakiwemo Mchungaji Dickson, Stanley, Mainah, Lukumay, Kyando na Wainjilisti na wengine wote kwa kazi kubwa waliyoifanya Gezaulole. Pia baada ya kuokoka mimi na waganga wengine na wachawi waliokoka kwa sababu mkubwa wao amesalimu amri.