MIAKA MIWILI BAADA YA KUTEKWA WASICHANA 276 NA BOKO HARAM, MMOJA APATIKANA AKIWA MJAMZITO


Kama unazikumbuka story za kundi la Kigaidi la Boko Haram kuteka wasichana 276 Nchini Nigeria, sasa leo taarifa zilizopatikana ni kwamba binti mmoja amepatikana baada ya miaka miwili.

Binti huyo kwa jina la Amina Ali amepatikana akiwa na ujauzito kwenye msitu wa Sambisa huko kaskazini mwa Nigeria ambapo ndipo walikuwa wamefichwa wasichana hao.

Wasichana hao ambao huitwa ‘chibok girls‘ ambao ni wanafunzi wa shule ya bweni walitekwa na magaidi hao wakiwa shuleni.