Select Menu

News

USIKOSE IJUMAA HII MLIMA WA MOTO MIKOCHENI "B"

USIKOSE IJUMAA HII MLIMA WA MOTO MIKOCHENI "B"

MLIMA WA MOTO JUMAPILI HII

MLIMA WA MOTO JUMAPILI HII

SARAH KUZINDUA ALBAM YAKE JUMAPILI HII

SARAH KUZINDUA ALBAM YAKE JUMAPILI HII

MCH. BURTON SANGA

MCH. BURTON SANGA

TTCL

TTCL

GEPF

GEPF

VIGAE TANGAZO

VIGAE TANGAZO

IRINGA MAZIWA TANGAZO

IRINGA MAZIWA TANGAZO

AZAM TV

AZAM TV

RUMAFRICA NA HABARI ZA GOSPEL: Bonyeza alama nyekundu kusoma zaidi

RUMAFRICA Online MAGAZINE: Bonyeza alama nyekundu kusoma zaidi

Rumafrica. Powered by Blogger.

RUMAFRICA Online TV: Bonyeza alama nyekundu kusoma zaidi

RUMAFRICA: MATANGAZO: Bonyeza alama nyekundu

ELIMIKA NA RUMAFRICA

RUMAFRICA MTAANI

MLIMA WA MOTO ONLINE TV NA HABARI MBALIMBALI ZA MLIMA WA MOTO

RUMAFRICA VIDEO

» » MLIPUKO WA SIFA KULINDIMA JUMAPILI HII


Sanga Rulea 9:52 AM 0


Baada ya kusubiri kwa muda mrefu nyimbo za zamani za kwaya maarufu nchini ya Tumaini Shangilieni ya jijini Arusha, hatimaye wapenzi wa muziki wa injili na wadau wa kwaya hiyo wanatarajiwa kupokea DVD mpya ya nyimbo za zamani iitwayo "SILAHA YA USHINDI" ambayo inatarajiwa kuzinduliwa rasmi jumapili hii jijini Arusha.
Kwaya ya Tumaini ambayo mpaka sasa ina DVD 5 mpaka sasa, haikutoa nyimbo za zamani tangu watoe DVD namba 2 iitwayo "Shangilieni part 2" ambapo kutokana na maombi ya wadau wengi kuzipata nyimbo hizo, kwaya hiyo imeitikia mwito na kukamilisha album hiyo ambayo inatarajiwa kufanyika baraka kwa wengi kama ilivyo kawaida ya nyimbo na matoleo yatolewayo na kwaya hiyo.
Uzinduzi huo unatarajiwa kuanzia ibadani kanisani kwao St James Anglikana Kaloleni kisha kufuatiwa na tamasha kubwa litakalofanyika kwenye ukumbi wa Metropole ulipo jijini humo wakisindikizwa na kwaya maarufu ya Kijitonyama Uinjilisti ya jijini Dar es salaam, kuanzia saa 8 mchana sambamba na wenyeji wengine kama Upendo choir St James Arusha waliotamba na DVD ya "Furaha Gani" mwanzoni mwa mwaka ya 2000.
Awali kabla ya uzinduzi huo kutakuwepo na tamasha lingine la awali ambalo litafanyika tarehe jumamosi tarehe 07 May 2016 FRANGPAN GARDEN karibu na Njiro complex au sabato njiro kuanzia saa 12 jioni. "Siku ya kwanza ni JUMAMOSI 7/5/2016 Namaanisha kesho kutwa. Hii itakuwa ni CHAKULA CHA JIONI. Mahali ni FRANGPAN GARDEN karibu na NJIRO COMPLEX au SABATO NJIRO. Lengo ni kuchangia ununuzi wa basi kubwa ili kurahisisha usafiri wa kundi lenye idadi ya waimbaji 82. Tunatamani tukisafiri tufike mahali pengi bila changamoto ya usafiri. MEZA YA WATU SITA NI TSHS 500,000. Wageni kwaya alikwa ni KWAYA YA UINJILISTI KKKT KIJITONYAMA - DAR ES SALAAM. kuanzia saa 11 jioni" Amesema John Mtangoo mmoja wa walimu na kiongozi wa kwaya hiyo.


Angalia moja ya nyimbo za zamani za Tumaini kutoka kwenye DVD yao ya kwanza


«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

JIUNGE NA ST MARY'S INT'L SCHOOLS

JIUNGE NA ST MARY'S INT'L SCHOOLS