MelK Premium Suits

TANGAZO MUHIMU

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BISHOP DR. M.E. ADMIN

BISHOP DR. M.E. ADMIN

SANDLANDS HOTEL KARIAKOO

NABII FLORA SIKU YA JUMAPILI 01.05.2016 ATOA UJUMBE MZITO NA KUFARIJI MIOYO YETUTunapokwenda kuingia mwezi huu wa tano lazima uvuke, naona BWANA anatengeneza njia ya kuvuka, ni lazima tutoke na vitu, lazima tutoke na watoto wetu tuingie mwezi Habu, mwezi huu wa tao tunakwenda kumiliki na kutawala, tunaingia kwenye nchi njema kwenye nchi ya asali na maziwa, siyo nchi kama hizi ulizozizoea, sasa unakwenda kuingia katika nchi upewayo na BWANA, unapoenda kubarikiwa na kufanikiwa amini neno la Bwana hi siku ya leo ni siku ya urejesho Bwana amesema anarejesha Baraka zako, anakwenda kubadilisha maisha yako leo, anakwenda kutenda muujiza kwako leo, kama ambavyo Bwana aligeuza uteka wa Ayubu, ndivyo Yesu anakwenda kuugeuza uteka wako, ndipo nilipoona BWANA akiniambia kwamba waambie watu wangu ninakwenda kuugeuza uteka wao, 
Nabii Flora (kushoto) na Mch. July

kama vile kwa Ayubu Bwana akaugeuza uteka wa Ayubu alipoombea rafiki zake, Bwana akambariki Ayubu kwa mara ya pili, ndipo akamzidisha sanan na akamfanikisha sanan watu waliokuwa wakijua kwamba Ayubu hatokuja kufanikiwa hata watu waliokuwa hawakutegemea kama Ayubu ataweza kuja kufanikiwa wakaanza kumshangaa wakasema ni wewe kweli au? 
Na hata wewe leo wat watakushangaa, umepita katika shida nyingi kwa muda mrefu, umepita katika ukame wa fedha, umelia kampuni yako imeyumba biashara zako haziendi, una mizigo mizuri sana lakini shetani ameleta mgandamizo, nakwenda kugeuza uteka juu ya Taifa langu la Tanzania, WANA alete Baraka katika nchi hii, alete Baraka katika kanisa letu, alete Baraka kwa watu mbali mbali. Kama Ayubu alivyoongezewa na Bwana nawe ninakwambi wewe ambaye umepita katika hali ngumu kwa muda mrefu, umekuwa ukila mlo mmoja lakini sasa hivi utakwenda kula ilo mitatu mikamilifu, Bwana akupe kula milo mitatu mikamilifu, nawezekana kwa BWANA, 
Daudi alipokuwa kwenye nchi iliyojaa ukame na njaa Daudi akatafuta uso wa BWANA akamlilia MUNGU, BWANA akageuza akayasikia maombi ya Daudi akainyeshea nchi yake. Nami BWANA asikie akainyeshee mvua ya fedha nchi yangu ya Tanzania, watu wanalia shida, watu wanalia maisha ni magumu, Bwana alete mema, Bwana alete mazuri katika nchi yetu ya Tanzania ,haleluya. 

AYUBU 42;10 Kisha BWANA akaugeuza uteka wa Ayubu, hapo alipowaombea rafiki zake, BWANA naye akampa Ayubu mara mbili kuliko hayo aliyokuwa nayo kwanza.

Wewe ni rafiki yangu katika Bwana maana hata Bwana Yesu ninakuombea mema kwa BWANA, ninakuombea BWANA akubariki, nakuombea BWANA ageuze uteka wako, nkuombea BWANA ageuze maiisha magumu alete masha mazuri kwako, kama Bwana Yesu anavyosema sisi ni marafiki wema kwetu na yeyey ni mpenzi mwema kwetu, na yeye ageuze uteka wako, mimi ninakuombea rafiki yangu ili uweze kubarikiwa, nakuombea il utajirike, 
nakuombea ili upate nauli ya kuja kumuabudu MUNGU, nakuombea usikose fedha Bwana alete mvua ya Baraka kwako, Bwna ageuze uteka wako, aumepita katika hali ngumu kwa muda mrefu, umehekwa na wenzako, kazii yako imetekwa, nafasi yako kazini imetekwa, sasa BWANA ageuze uteka wako, Bwana arejeshe Baraka zako leo, arejesha mahusiano yako leo, arejeshe uchumi wako leo, arejeshe afya yako leo, arajeshe mchumba wako leo ametekwa katika ulimwengu wa kirorho akikuona anakuogopa, ukimuona unamuogopa, 
mchumba wako akikuona mwanaume anaiinamisha kichwa chake chini saa ngapi ndoa itatokea, Bwana arejeshe uteka wako leo, ageuze uteka kwako, ageuze maisha yako, kama Bwana alivyeuza uteka kwa Ayubu name nakuombea Bwana ageuze uteka kwako nataka Bwana akubariki, hali ya kutokuzaa, hali ya kutokuolewa nnakuombea Yesu ageuze uteka kwako leo alete Baraka inawezekana kupata Baraka mama. 


Kama ambavyo Ayubu alizidishiwa mara mbili na ulikuwa unasalimiwa na sasa wewe ninakuombea ukapate kibali mara mbili zaidi na mara dufu kwako, ulikuwa unaingia sehemu heshima inatokea sasa Bwana alete heshima kwako mara mbili zaidi, alete kibali mara mbili, arejeshe upako mara mbili, arejeshe pesa mara mbili, alejeshe afya yako mara mbili, alejeshe ushindi mara mbili, alete wateja mara mbili, Bwana anakwenda kukupa mara mbili kama ambavyo hata Ayubu aliongezewa mara mbili, anakwenda kupanua wigo wa kampuni yako, anakwenda kupanua wingi wa pesa zako, unakwenda kufanikiwa, anakwenda kukupa mara mbili leo,
 nasema hatutakufa mpakak BWANA ametubariki, tunakwenda mwezi wa tano hatukubali mpaka Yesu atende kitu kwetu na sisi, kama alivyombariiki Ayubu na aliweza kumpa mara mbili, na mimi ninasema BWANA ageuze uteka wako umedharauliwa vya kutosha, mpaka marafiki wamekubeza wanasema huyu naye hata kutuchangia na sisi yeye kila siku tu, BWANA arudishe heshima yako mara mbili, Yesu alete Baraka zake kwako mara mbili, arudishe vitu vyako mara mbili, arudishe kibali chako mara mbili, arudishe heshima yako mara mbili, arudishe nguvu ya maombi mara mbili, arudishe kila kilichopotea mara mbili, natangaza habari njema mara mbili. 

Kama alivyombarikia Ayubu mara mbili na vikaongezeka na wewe Bwana akuzidishie Baraka akuongezee mara mbili, Bwana ageuze uteka wako umedharauliwa vya kutosha ni wakati wa BWANA kukuinua, Bwana kanituma kwako nikwambie unakwenda kunuliwa, maisha ya kuzug zuga yanatosha, maisha ya kuranda randa yanatosha, maisha ya kubahatisha yatosha, maisha ya kuishi kama kipofu yatosha, huu ni wakati wako wa kutendewa, 
kaka Bwana alivyompa kibali Nabii Elisha akamtosa kwenye moto adui na mimi leo ninamtosa kwenye moto adui aliyekamata kibali chako, aliyekamata uchumi wako tunamtakasa kwenye moto, achia huu uzao, achia uchumi wao, achia wazee wa kanisa, achia, nakutaosa kwenye moto, achia mkno ya watu hawa wafanikiwe, achiauchumi wao wafanikiwe, achia elimu, achia vyote, ninamteketeza Yule adui aliyekutesa. Name naachia ili Bwana akupe mara mbili, name nageuza mabaya yote, nageuza bahati mbaya, hautazaa tena mtoto akafa. SHUHUDA

MTOTO APONYWA KWA KUTUMIA SABUNI;
Kwa jina naitwa Prosper Mbugi ni mzee wa kanisa hili, nilikuwa na mgonjwa alikuwa amelazwa katika Hospitali ya Mlalakua Mwenge na alikuwa amelazwa kwa muda wa miezi sita na alikuwa ameanza kuisha kwa kula kwa kutumia mpira mimi nikachukua ile sabuni nikampa mama yake nikamwambia mama yake amuogeshee na maji umpe anywe baada ya siku tatu nilikuta mtoto amechomoa ule mpira wa kulia chakula na ameutupa baada ya kutumia sabuni hiyo, kwa kweli MUNGU ametenda.
MATUKIO YA PICHA

Nabii Flora (kushoto) na Mch. July