RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

PAPA-KILA MKRISTO ALIYEBATIZWA ANAWAJIBU WA KUMTANGAZA KRISTO KILA MAHALI

Baba Mtakatifu Francisko, amehimiza Wakristo kumhubiri Kristo, kila mahali duniani bila woga.

Himizo hilo amelitoa mbele ya maelfu ya mahujaji na wageni waliokusanyika katika Uwanja wa Kanisa Kuu la Mtakatifu PetroLilopo Vatican Nchini Italy, ambayo pia ilikuwa ni siku ya maadhimisho ya Sikukuu ya Kupaa kwa yesu kristo .

Akitoa hotuba fupi juu ya siku kuu ya Kupaa Yesu kristo , Papa amesema, “awali kabla ya kuwaacha marafiki zake , Yesu alifanya rejea katika kifo na ufufuko wake , akisema ninyi ni mashahidi wangu. Na kumbe Yesu anawataja mitume wake waliokuwa mashahidi wakati wa mateso kifo na ufufuko wake pia wanakuwa mashahidi wake wakati wa kupaaa kwake Kristo”

Baba Mtakatifu aliendelea kusema, “Kwa kweli, baada ya kuona Bwana wao anapaaa mbinguni, wafuasi walirudi mjini, wakishuhudia kwa furaha na guvu zote kama mashahidi, walivyomwona Yesu akipaa mbinguni.


Kwa furaha walitangaza hilo kwa kwa kila mtu, na juu ya maisha mapya yanayoletwa na Kristo Mfufuka,na katika jina lake, walihubiri katika mataifa yote, toba na msamaha wa dhambi.

Baba Mtakatifu aliendelea kusema, walikuwa mashahidi si kwa maneno tu lakini pia kwa matendo katika maisha ya kila siku.

Na hivyo Papa akatoa wito kwa wabatizwa wote wa Kristo akisema, ni kutoa ushuhuda kila siku, kama inavyotangazwa na Makanisa kila Jumapili na kuendelea kwa wiki nzima, katika nyumba zetu, ofisi zetu, shule zetu, kukusanywa kwetu maeneo na kumbi za burudani, hospitali zetu, magereza, na nyumba kwa ajili ya wazee, katika maeneo inaishi wahamiaji, nje na ndani ya miji.

Amesema lazima kupeleka ushuhuda huu kila wiki kwamba Yesu kapaa mbinguni , lakini yu pamoja nasi. Kristo ni hai!

Pia Papa wakati huo wa sala la Malkia wa Mbingu , aliwakumbuka Wamama wote duniani, kwa kuwa pia ilikuwa ni Siku ya Dunia ya kuwaenzi wamama wote, wenye watoto hata wasiojaliwa watoto.