RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

PICHA ZA WATUMISHI WA UBALOZI UINGEREZA WALIPOAGWA NA WANA AFRIKA MASHARIKI

Angalia picha za matukio ya jumapili iliyopita wakati waumini katika kanisa la St Anne's Lutheran jijini London nchini Uingereza, walipowaaga rasmi waliokuwa watumishi wa ubalozi wa Tanzania nchini humo ambao kwa sasa wanarajea nyumbani kwa kazi nyingine. Walioagwa ni pamoja na mke wa aliyekuwa Balozi Peter Kallaghe pamoja na ofisa ubalozi bwana na Bi Kiondo.

Ibada hiyo ilianza saa 8 mchana na kumalizika saa 11 jioni ambapo licha ya zawadi na maombi kwa watumishi hao, pia kama ilivyoada ya ibada kanisani hapo huwa watu wanaokumbuka siku yao ya kuzaliwa hufanyiwa maombi maalumu pamoja na kutayarishiwa keki. Ambapo jumapili iliyoisha tukio hilo lilikuwa kwa wazaliwa wa mwezi April na May. 

Ibada katika kanisa hilo hufanyika kila jumapili ya mwanzo wa mwezi na jumapili ya tatu ya mwezi huwa siku ya kuichambua biblia ama Bible Study. Ibada zote huanza saa 8 mchana hadi saa 10 jioni.
Picha ya juu na chini ni Mchungaji kiongozi ibada ya kiswahili, Moses Shonga akizungumza jambo



Waliokuwa wanaadhimisha siku zao za kuzaliwa kwa mwezi April na May


Baadhi ya waumini




Bwana na Bibi Kiondo wakisikiliza neno la kuagwa kutoka kwa mzee wa kanisa

Mzee Kiondo akizungumza ibadani hapo huku akimwangalia mkewe kuitikia anayosema






















Picha ©Rori Masiane

- See more at: http://www.gospelkitaa.co.tz/2016/05/picha-za-watumishi-wa-ubalozi-uingereza.html#sthash.05HrdVcZ.dpuf