RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

STARA THOMAS AZIDI KUUKULIA WOKOVU, AJIPANGA KWA ALBUM YA PILI YA GOSPEL

Stara ThomasStara Thomas mwanamama nguli wa muziki nchini ameiambia Hosanna Kwanza kuwa jumatatu ya kesho 16/5/2016 atakuwa akianza rasmi kurekodi album yake ya pili kwa nyimbo za injili.Stara Thomas kabla ya kumrudia Mungu alikuwa akifanya Secular Music na kujipatia umaarufu mkubwa nchini ndani na nje ya nchi.

Baadaya kuokoka Stara aliarecord album ya nyimbo za Injili alioiita NANI MSHAMBA na alifanikiwa kurekodi Video nne za album hiyo.Kwa sasa Stara anasema project hii atafanya avideo zobe baada ya Audio kukamilika kasha uzinduzi utajumuisha album zote mbili ya kwanza nay a Pili.


Stara Thomas Akiwa na Masanja kwenye moja ya matamasha ya Injili


Akizungumza na Hosanna Kwanza kuhusu maisha ya wokovu na muziki wake anasema, “kwa sasa nimekua kwenye wokovu na viwango vimepanda,hapo mwanzo sikua na jua vitu vingi kuhusu wokovu na pia sikuwa na connection kubwa kwenye Gospel ila kwa sasa nmepanuka”.Stara alizidi kusema hata kwenye muziki wangu wa injili sasa hivi sifanyi vitu peke yangu niko na watumishi wa Mungu amabao tunashauriana nao kabla sijafanya jambo.Stara Thomas kwa sasa anasali kanisa la TAG Kimanga kwa mchungaji MALEGO.