RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

ULIFIKIRIA KUJIAJIRI?







.




11:46 AM by nimfa richard2 comments

Kumekua na tatizo la ajira kutokana na idadi ya wasomi kuongezeka;Ukiachana na watu (wasomi na ambao hawajasoma) waliopanga kujiajiri katika maisha yao toka siku nyingi.Wengi sana wanatamani kujiajiri lakini wanashindwa au wanakua na uoga Fulani.


Ili utimize malengo yako yakujiajiri unapaswa:

Kua na uthubutu
Unatakiwa usiwe muoga kugeuza malengo yako katika matendo.Wengi wamekua na mawazo mazuri ya biashara au huduma Fulani lakini anashindwa kwa kuwaza siwezi au sintafika mbali.Ondoa hizo fikra maana zitakuangusha katika kutimiza malengo ya maisha yako.

Kuwa tayari kupata faida au hasara
Unapogeuza mawazo katika utendaji hasa wakukuingizia kipato usifikirie upande mmoja tu yaani faida.Jua biashara au huduma yoyote inahitaji kila jitihada kuweza kuifanya ikubalike na kupendwa na watu(wateja).Kadhalika kuna saa mtu anafanya kitu kama unachokifanya(ushindani) hivyo kupelekea kugawana faida au kukunyang’anya yote nakukupelekea kwenye hasara.Sasa kama ulifikiria upande wa faida tu itakufanya udhani biashara unayofanya haifai hivyo kuachana nayo.Ni vizuri uwe tayari kwa pande mbili;faida na hasara.


Kukumbana na lawama

Unapoanza kufanya shughuli yoyote ya kipato kuwa tayari kupata lawama kutoka kwa; aidha wasaidizi wako/wafanyakazi au baadhi ya wateja.Ni vizuri ukapiga moyo konde na kujitahidi kutatua yale yanayowezekana kwa haraka hasa kwa wateja.Vile vile sio watu wote wanapenda mafanikio ya wenzao,wakati mwingine wasaidizi wako wanaweza kukupa lawama mbalimbali na kuathiri moja kwa moja mipango yako ya biashara.

Kuwa tayari kupokea ushauri wa kuvunja moyo
Hapa ndipo pakua makini.Kila mtu atakuambia lake,mwingine anaweza akuambie, ``hiyo biashara yako kila mtu anafanya” mara ``wewe hauwezi kabisa, kwa ninavyokujua?” n.k.Ni vizuri uwe tayari kwa hayo yote muhimu ni UTHUBUTU na utayari wako.

Penda,thamini na jali unachokifanya
Ukiipenda kazi yako,hautakata tamaa na utaifanya kwa ufanisi zaidi na itakua rahisi kupata mawazo mapya ya maboresho.

Unapopata nafasi jiendeleze kwa utaalam zaidi kuhusiana na unachokifanya(haijalishi umesomea au haujasomea)

Hii itakusaidia kukabiliana na mabadiliko yoyote ya sayansi na teknolojia.Vile vile maboresho ya kiutendaji na katika uuzaji wa bidhaa au huduma zako. 

Usiridhike na ulipofikia ,tamani kukua zaidi katika unachokifanya ilimradi usidhulumu mwenzako au kuiba(fanya vitu kwa uhalali si machoni pa watu tu bali hata mbele za Mungu)

Wengine walianza kama wamachinga lakini wakafanikiwa mpaka hatua yakumiliki au kukodi nyumba ya biashara yote hayo ni kutokana na kutoridhika kua mmachinga(alipoanzia) ni kwa ajili ya mawazo ya maendeleo toka alipokua na uthubutu wa biashara yake.

Fanya mkopo kua ni kwa ajili yakujazia mtaji na usiwe ndio mtaji

Unapoliweka wazo katika utendaji wa kukuingizia kipato inabidi uwe ulishajipanga kuwa na walau mtaji wakuanzia ili unapoona unahitaji msaada ndipo ukakope na hapo inabidi ujue kwanza muelekeo wa biashara upoje yaani upo palepale au unapanda kwa kasi au taratibu.Hii itakusaidia kujua utachukua mkopo kiasi gani na marejesho ya aina gani yatakufaa kulingana na biashara yako.Au uongeze bidhaa gani itakayosaidia bidhaa nyingine kutoka ambapo ndipo utachukua mkopo kwa ajili hiyo.Kujipanga katika biashara ni muhimu sana.Umakini wa mikopo uwepo kwa sababu unaweza kukuingiza katika hali ya stress na hatimaye magonjwa.