RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

WAIMBAJI WAZAWA WA JOYOUS CELEBRATION KAZI ZAO ZAANZA KUKUBALIKA ZAIDI


Sibusiso Mthembu
Baada ya waimbaji wawili wa kigeni wa Joyous Celebration kutamba kwa nyimbo zao kutazamwa zaidi kwenye mtandao wa YouTube, hatimaye waimbaji wazawa nao wameanza kufuata nyayo za waimbaji hao baada ya nyimbo zao kutazamwa zaidi ya millioni moja katika mtandao huo.

Waimbaji waliovunja rekodi ya kundi hilo wa kwanza ni mchungaji Agu Uchechukwu ama mwite Pastor Uche raia wa Nigeria mwenye makazi pia Afrika ya kusini alivunja rekodi kupitia wimbo wake wa 'My God is good, ambao unapatikana katika DVD ya 13 ya Joyous ambapo mpaka sasa wimbo huo umetizamwa mara millioni 4,207,468 akifuatiwa kwa karibu na Mzimbabwe Mkhululi Bhebhe na wimbo wake wa kwanza Tambira Jehova ambao aliuimba katika DVD ya 15 mpaka sasa umetazamwa mara millioni 4,071,214.



Mercy na mumewe Sipho


Kwa upande wa waimbaji wazawa ambao kwa kawaida nyimbo zao awali zilikuwa hazifikishi hata watazamaji laki tano, mwanadada Mercy Mndlovu Manqele alikuwa wa kwanza kupitia wimbo wake wa Hihanya Mahala alioimba katika DVD ya 16 ambapo mpaka sasa umetazamwa mara millioni1,682,528. Na ndiye mwimbaji mzawa wa Afrika ya kusini aliyepata mwaliko wa kimataifa angali akiwa na kundi hilo kwenda kwenye huduma Amerika ya kusini.

Kwasasa kijana ambaye ametokea kupendwa zaidi na mashabiki wa kundi hilo kwa uchezaji, uimbaji na nyimbo zake Sibusiso Mthembu aliweza kufikisha watazamaji millioni 1,147,399 kupitia wimbo wake wa Haleluya Nkateko unaopatikana katika DVD ya 19 chini ya anuani ya VEVO ya kundi hilo, hata hivyo kupitia anuani ya shabiki wa kundi hilo aliyeweka wimbo mwingine wa kijana huyo uitwao Ngino jesu tayari unawatazamaji millioni 1,147,399
Hata hivyo kijana Mkhululi Bhebhe bado ndiye anashikilia usukani wa nyimbo zake zote tano kutoka


Pastor Uche


DVD ya 15 hadi ya 19 kufanya vizuri kwa kutazamwa kwenye mtandao huo kwakupitisha watazamaji zaidi ya laki tano huku pia wimbo wake mpya wa 6 kutoka DVD ya 20 bado haujawekwa kwenye YouTube yawezekana pia ukapokelewa vizuri na watazamaji wa kundi hilo ambalo linazidi kupata mashabiki wapya kila kukicha sambamba na nyimbo zao kuanza kupata mashabiki kwenye mitandao ya kijamii. Hata hivyo Mercy pamoja na Uche walishamaliza mkataba na kundi hilo. 

Source: Gospel Kitaa