MelK Premium Suits

TANGAZO MUHIMU

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BISHOP DR. M.E. ADMIN

BISHOP DR. M.E. ADMIN

SANDLANDS HOTEL KARIAKOO

YNA WA THE PROMISE AWEKA PEMBENI UIGIZAJI AJIKITA KUMCHA MUNGU NA KULEA FAMILIA YAKEKristine Hermosa Sotto na familia yake


Ili kuonyesha kwamba anafuraha tele na maisha yake ya ndoa, mwigizaji nyota wa Ufilipino ambaye ameokoka, Kristine Hermosa almaarufu kama YNA katika tamthilia ya The Promise, ameamua kujikita zaidi na familia yake baada ya kutangaza anatarajia kupata mtoto wa tatu katika ndoa yake na mwigizaji mwenzake Oyo Boy Sotto.

Mwigizaji huyo aliamua kutangaza ujauzito wake mpya hivi karibuni, wakati ambao mashabiki wake


Jericho na mkewe Kim


walitegemea kumuona akirudi tena kwenye uigizaji baada ya mtoto wake wa pili aitwaye Kaleb Sotto kuanza kutembea. Aidha mashabiki hao walikuwa na imani ya kumuona mwanadada huyo amabye yeye na mumewe ni wafuasi wazuri wa wokovu, baada ya mpenzi wake wa zamani ambaye kwasasa ni mume wa mtu Jericho Rosales almaarufu kama Angelo kuwa tayari kuigiza tena na Kristine na kwamba wanatarajia jambo hilo kutokea karibuni.

Hata hivyo msimamo wa binti huyo kuweka familia yake mbele dhidi ya fani yake umepokelewa na kupongezwa na wengi licha ya kuumia kumkosa kwenye uigizaji, wakidai kwamba ni msichana wa kuigwa nchini humo kutokana na tabia nzuri aliyonayo, na kuachana na umaarufu na kuweka mbele familia yake. Kristine na mumewe Oyo wamejaaliwa watoto wawili mpaka sasa kwenye ndoa yao pamoja na mtoto mwingine wa kiume waliyemchukua kutoka kituo cha watoto yatima ili kumlea, na kufanya kuwa na idadi ya watoto watatu mpaka sasa huku mtoto mwingine yupo mbioni.
Familia ya bwana na bibi Oyo Boy Sotto, maalumu kwa kijana wao alipotimiza mwaka mmoja


Source Gospek Kitaa