MelK Premium Suits

TANGAZO MUHIMU

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BISHOP DR. M.E. ADMIN

BISHOP DR. M.E. ADMIN

SANDLANDS HOTEL KARIAKOO

08.06.2016: MCH. NOAH LUKUMAY ALIVYOHUBILI JUU YA KUTEMBEA NDANI YA NEEMA

Mch. Noah Lukumay aliweza kufundisha juu ya watu kutembea ndani ya neema ya Bwana katika ibada iliyofanyika Mlima wa Moto Mikocheni “B” jijini Dar es Salaam kwa Bishop Dr. Gertrude Rwakatare siku ya Jumatano 08.06.2016 na alikuwa na haya ya kusema, Neema ni nini? Neema ni kitu ambacho hujagalamia. Kuna watu wengine waliingia katika kinyang’anyilo cha Ubunge wakapambana kupata ubunge, kwa sababu hiyo kuingia kwao bungeni sio ni kwa neema kwasababu kuna nguvu Fulani walitumia kuingia bungeni. Lakini kuna tu mwingine ambaye alikuwa tu nyumbani kwake anafanya kazi zake kama kawaida lakini ghafla jina lake likatajwa na Mh. Rais Dkt. John Pombe Magufuli kuwa yeye ni mmoja ya wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. 

Mch. Noah Lukumay

Mtu huyo hajaenda kwenye kampeni, hajaenda kuomba kura, hajaenda kumwambia Rais, hajaenda mahali popote kuwa anahitaji nafasi hiyo ya Ubunge kwahiyo huyu mtu tunaita amepata Neema. Inawezekana katika nafasi hiyo ya Ubunge kulikuwa na watu wengi sana ambao wangefaa, lakini wewe umeangukia katika hiki kitu tunachoita “Neema”.
Kwahiyo Sio wote wanaoshindana wanashinda kwenye mashindano bali kuna bahati inamuangukia kila mtu kwa nafasi yake. Tusipoongelea neema tutashindwa kuona nguvu ya Mungu katika maisha yetu, kwasababu Neema ya Mungu ikipungua katika maisha yetu shina la uchungu linaota, yaani kuna nguvu nyingine inatokea ukipungukiwa na Neema.

Neema ni ile hali ambayo unapita pasipokujitahidi au unapita sehemu ambayo ulidhani hutaweza kupita. Ni sawa leo wewe ukaitwa “First Lady au mke wa Rais” lakini hujui ni juhudi gani ulizifanya kuitwa “First lady” Kwa mfano mke wa Evander Holyfield (mwanamasumbwi) anakula matunda ya mume wake Evander Holyfiend na sio yeye aliyepiga na kupata pesa nyingi, ila kuna mtu aliyepigana kwasababu yake. Na ndio kanisa la leo tunashindwa kutambua kuwa kuna mtu amepigana kwasababu yetu, na huyo mtu ni Yesu Kristo aliyepambana kwaajili yetu.

Hii inamaanisha kuwa bondia anapigana ngumi na ushindi unakuja ndani ya nyumba. Na yule ambaye yuko nyumbani kwa huyo bondia atafurahia na kujivuna na kusema na yeye ni miongoni mwa washindi hata kama hajui hata kurusha ngumi, na hii ni kwasababu kuna mtu mmoja kwenye familia au ukoo amepigana na kushinda ili watu walionyuma yake nao wafurahie ushindi wake na kula matunda yake.

Na sisi kama kanisani tunapewa neema na Mungu na hiyo neema haijatokana na nguvu zetu bali ni neema ambayo ilishalipiwa msalabani, na hiyo neema imeshaachiwaliwa kwaajili yetu. Hatuna haja ya kupambana kwasabu Yesu ameshapambana kwaajili yetu, hatuna haja ya kushindana kwa maana Yesu ameshashinda, kazi yetu ni kushangilia ushindi kwasababu neema iko ndani yetu. Sisi walokole tunapaswa kutambua kwamba, sisi ni watu

Neema inachanganya matatizo inakuwa miujiza, neema inageza mambo mabaya yanakuwa mazuri. Kama unahitaji neema ya Bwana sema, “Nahitaji Neema ya Bwana ishue juu yangu kwa Jina la Yesu”. Neema ya Bwana ikishuka hali ya hewa inabadilika. Hata unavyokula na kuvaa ni kwa neema ya Mungu umepata. Na mimi imeshatendeka katika ulimwengu wa Roho, hatuajapokea kimiujiza ila tumepokea kwa neema ya Bwana iliyoachiliwa kwetu tunayemjua Yesu.
Neema inaweza kujibu maisha yako pasipo wewe kushughulika. Neema haiitaji refa, au mtu akusukume, haiitaji mtu wa kukusaidia. Ukiwa unajua neema ya Mungu, na ukaanza kujiuliza utafanya nini kwa kutumia akili yako basi ujue tayari umepoteza neema ya Mungu. Watu wengi wamepoteza Neema ya Mungu kwasababu hawajaitambua. Wenzetu wa “West Africa” huwa wanasema, “Kwa neema ya Mungu nimeamka” (By the Grace of God Im fine), by the grace of God nimepata gari. Hii ni kwa maana kwamba kununua gari si kwasababu ya pesa, kwasabu wapo watu wana pesa nyingi lakini hawanunui magari, kujenga nyumba si kwasababu ya fedha ila ni kwa neema tu inashuka juu yako na mambo yananyooka.

Kujuana na watu sio kwasababu unaongea sana ila ni kwa neema tu ya Mungu inatokea na ukajikuta unafahamika sana kuliko watu wengine na sio kwamba una akili sana kwasababu kuna wenye akili kukuzidi wewe, kuna wenye ufahamu kukuzidi wewe ila kuna neema imekuangukia. Kuolewa sio uzuri kwani kuna wazuri kukuzidi wewe na hawajaolewa, ila hiyo ni kwa neema tu. Kungekuwa ni uzuri, wengi wasingeolewa, kuna wasichana wengine sura sio nzuri lakini wameolewa, unaanza kujiuliza huyu jamaa alipendea nini kwa huyu msichana, na usijui huyu msichana ana neema na ndio maana amechanganya huyu jamaa na kuweza kumuoa.
niasema, “Pokea hiyo neema kwa jina la Yesu Kristo, pokea katika biashara zako kwa jina la Yesu, . Natamka kuwa wengine wakashindwe na wewe ukafanikiwe kwa jina la Yesu, watoto wako wakafaulu, wakati watoto wengine wanafukuzwa ada wa kwako wakabaki wanasoma kwa jina la Yesu.”

Kuna watu wengine walikuwa wajinga darasani lakini walikuwa wanapendwa sana darasani hata kama ni wajinga, wengine ni maskini nyumbani kwao lakini bado watu wanawapenda na umaskini wao, na unaanza kujiuliza kitu gani wanapendea kwa watu hawa ambao hawana lolote? Ila unasahau kuwa huyu mtu amekosa kila kitu ila ana neema ndani yake.
Heri ukose kila kitu ila omba neema iingine ndani yako iwe msingi wa maisha yako. Ukiwa na neema hata kama maisha yako hayasomeki ila mbingu itabadilisha maisha yako. Watu wanaweza wakawa hawakuelewi lakini viatu vya neema ulivyovaa vinakuwa na nguvu katika maisha yako. Ukishakuwa na neema, unatoka kwenye matatizo unaingia kwenye Baraka, unatoka kwenye umaskini unaingia kwenye utajiri. Leo kama mtumishi wa Mungu ninakuahamisha kutoka kwenye kudhalilishwa na kuingia kwenye kuheshimika. Leo ninakutoa kutoka kwenye magonjwa na uingie kwenye afya, na kama unaamini sema fireeee!!!

Neema sio kitu cha kawaida, neema haujitahidi. Kuna watu wengine wanapiga kifua na kusema, “mimi ninafunga mara tatu”, “mimi ninafunga tatu kavu”, “mimi ninasoma sana Biblia”. Ndugu yangu wewe, neema haitokani na juhudi zako. Wengine wanasema “mimi nina “degree” tatu za Biblia”, hiyo sio Neema, ila hiyo ni jitihada zako au juhudi yako.

Neema haitembei na mtu ila inatembea na mtu anayesema, “Ninahitaji Bwana aniwezeshe kwa maana siwezi kwa akili zangu, siwezi kwa mawazo yangu, siwezi kwa ngu zangu bali ninahitaji Bwana anisaidie. Ukiona unaanza kujiona wewe unaweza sana kwa kutumia juhudi zako, basi ujue neema imepungua kwako. Ukiona umefikia mahali unajigonga kifua basi ujue neema imepotea kwako. Walokole wengi wamepoteza Neema kwasababu ya kiburi cha uzima, utaona mtu huyu ameinuka kidogo kiuchumi au kwa jambo lolote na anaanza kudharau Neema.
Unakuta huyu mtu anafanya kitu ambacho hakina hata sura wala hakisomeki katika jamii kwasababu hukujua kuwa uliingia kanisani ukinyenyenyekea na ulipofika kanisani Mungu akakuinua kidogo ukasahau kuwa ni kwa neema na ukaanza kusema, “Kumbe ni akili zangu tu”. Mtu huyu hata ukimsalimia Bwana Yesu asifiwe, anaanza kukujibu kwa bali sana au anakujibu huku akifanya mambo yake.

Dr. Gertrude Rwakatare nihubiri madhabahuni huwa naona kama kuna kitu ndani yangu kinanitesa sana. Utaona watu wengine wanafurahi lakini mimi sicheki, amani imetoweka nabaki ninatetemeka sijisikii raha, siku zingine ninakaa ofisini kwangu naona nakosa amani ninahitaji Bwana anaiwezeshe kwani siwezi kuongea na watu peke yangu, ninahitaji ile Neema ya Bwana kuwa juu yangu ili kila kitu kutoka kwa Mungu kishuke kupitia kinywa changu.
Kwa maana hatuweza kuongea kwasababu ya wingiu wa vitabu, kuna muda mwingine unafungua Biblia na unaona huelewi, unaanza kusema “Fungua Walaka wa Goliati”, watu wanaanza kushangaa hiyo Walaka wa Goriati iko wapi? Unaona maandiko yote yamepotea, unabaki unasema, “Hawa jamaa walikosea kuandika Biblia” Ila kwasabau hujasimama na neema ua Mungu na kuongea hujui umekosa Neema ya Bwana.
Kufanya kwako kazi kuwe kwajili ya Bwana, kuimba kwako usiimbe kwasababu unajua nyimbo, ila uimbe kwasababu unajua ni neema, kupiga vyombo vya muziki usipige eti kwasababu uanjua kupiga vyombo ila ujue ni kwa neema, tambua uko na Mungu wako aliye hai. Neema ya Bwana haitokani na juuhu au bidii yako baliNeema ya Bwana ni bure. Na usipoijua kuwa neema ya Bwana ni bure unajikuta unaenda kushoto na huendi kulia kwasababu ile Neema ya Mungu hujaitambua.

Nakuomba uipe nafasi Neema. Kuna watu wengi wameshindwa kuokoka sio kwasababu hawapendi bali wanapenda kuokoka na kusimama na Yesu lakini Neema haipo ndani yao. Na ndio maana wewe uliyeokoka usiwe wa kwanza kuwahukumu watu ambao hawajaokoka na kuwaona hawafai na kuanza kuwakanyaga walioshindwa kwasababu hata wewe unaweza kurudi nyuma na kuwa kama wao. Sio kuwa umeweza kuomba na kufunga ukashinda bali kuna Neema ya Mungu imekuangukia ukaweza.
Usiwe wa kwanza kuwahukumu watu bali waambie waifuate hiyo Neema ya Mungu na wakishaokoka, wakafunga na kuomba wajue kumbe haya yote yanafanyika ni kwa Neema. Hakuna mtu anayependa kushindwa, kila mtu anapenda kushinda. Naomba sasa ufuatishe maneno haya, sema, “Bwana Yesu, Neema ya Bwana ishuke juu yangu kwa jina la Yesu” Watu wanampenda Mungu, lakini Neema ya Mungu imepungua kwao, ikaota shina la mabaya wakaanza kupenda vitu vya dunia wakaacha kumpenda Mungu, wakashundwa kutembea kwenye Neema hii.
Nuhu alipata kibali, alipata neema, Mungu akamchagua katikati ya watu wote, na alipopata kibali, Mungu ankasema, “Nenda ukawape watu Neema hii”, baada ya kuambiawa hivyo, Nuhu hakunyamaza bali alitoka na hiyo Neema na kwambia watu kuwa mimi najenga Safina kwasababu Mungu amenambia, na amesema anakwenda kuiharibu dunia. Watu wakaanza kumdharau, lakini Nuhu hakuacha kuwaambia bali aliendelea kuongea nao. Nataka sasa nikuulize kuna watu ambao wamepata neema, hata kama familia yake inapotea lakini yeye hatapotea na kumuacha Yesu, hata kama wataingia gizani lakini yeye atabaki nuruni. Unatakiwa kuujiuliza kuwa ukipata hiyo Neema ya Mungu utaitumiaje

Mungu alimwambia Musa kuwa wale watu hawafai wacha tuwafute wote halafu tutengeneze mkataba Mimi na wewe. Mtu mwenye neema hataki wenzake wapotee. Musa akamgeukia Mungu akamkasilikia, akasema, “Ikiwa Mungu unampago wa kuwafuta wale basi anza na mimi, kwa maana kama wale wametenda dhambi na mimi ni miongoni mwao, usinitoe katikati yao kwasababu wale ninawajua ni wa aina gani”. Mungu akamwangalia Musa, akamwambia, “Mara nyingi watu hawafutwagi ila ni dhambi zao tu”.

Mungu aliweza kushusha Roho na kuwa mpole kwa Musa kwasabau Musa alikasilika kwasababu Mungu huyo huyo amewachukua watu hao kutoka jangwani na kuwavusha mahali na sasa MUNGU huyo huyo anataka kuwafuta, Je, watu watamuelewaje huyu MUNGU?” Musa akasema, Mungu kama unawageuka hawa watu basi hata mimi utanigeuka. Mungu akafikiria na kusema, kwasababu hiyo mimi Mungu sitawafuta.

Ni watu wangapi wanawabeba watu kwa Neema ya Mungu waliyonayo? Acha wewe kuichezea hiyo Neema ya Mungu uliyonayao, maandiko yanasema, “Usiichezee hiyo Neema uliyopewa na Bwana”. Nafasi uliyopewa sio ya kawaida, unayo “Access” ya kupanda mbinguni na kuachilia miujiza, na mimi ninasema, “Acha kukaa na miujiza”
Kuna watu wengine wanajiuliza, “Hivi tumtoe Mch. Noah Lukumay katika nafasi ile ya Uchungaji Kiongozi?”, watu wengine wanaanza kusema, “Ni kweli naona ni vyema tukamtoa kwasababu naona mambo yake sio mazuri, tumtoe tu?” Unajua ni kwani watu hawa wansema haya yote?, Neema waliyonayo ya kuwa viongozi wa maamuzi wanaitumia vibaya ya kutaka kumtoa Mch. Noah Lukumay.

Usitumie Neema yako vibaya, bali neema yako beba kwa watu walioshindwa, wasaidia watu walioumizwa, wangange moyo watu ambao hawawezi, wasaidie na wengine ili Neema yako izidi kukua na kuitumia katika nafasi yako. Watu wengi Neema zao zimekufa kwasababu wanaibeba pasipopaswa..

Sema, “Kwa jina la Yesu kuanzia leo, neema ya Bwana iwe ndani yangu kwa jina la Yesu. Ee Bwana Yesu Neema yako iingie kwangu kwa jina la Yesu. Kuanzia sasa Roho ya kukataliwa haina nafasi tena kwa jina la Yesu”
“Ninachotaka kusema ni kwamba, ukiwa na Neema leo utapita jangwani lakini unaelekea nchi ya Ahadi yenye maziwa. Leo unaona unakwenda kuishiwa, lakini hutaishia hapo kwasababu unakoelekea ni kwenye utele na asali kwasababu unayo Neema. Hata kama watu watakukimbia usiogope, watakufuata mahali ulipo, hata kama fedha imekukimbia usiogope, maadam unayo neema utakula, kwasababu kwa Potifa kuna chakula, kunakumiliki.

Waache wakutenge maadamu unayo neema, watakutupa kwenye shimo, neema itakutoa kwenye shimo, watakutupa chini, neema itakuinua juu, watakutupia majini nayo yatageuka kuwa muujiza wako kwasababu wewe sio wa kawaida, unayo neema ndani yako. Hauishi kwasabau una chakula, bali ni kwa neema ya Mungu. Mimi mchungaji wako Noah Lukumay nimeishi katika maisha ya umaskini uliokithiri.
Miaka ya nyuma kwetu, mafuta ya koroboi (kibatali) yakiisha unachukua tairi la gari unachoma moto na hapo hapo tunaishi nyumba ya majani. Moshi mkali na harufu ya tairi inanuka na sisi tupo ndani ya hicho kinyumba cha majani. Mnakaa humo ndani na hakuna anayeumwa, hakuna anayepata ungonjwa wa TB. Kukicha unatakiwa kuswaga mbuzi, ng’ombe, kondoo na punda na katikati ya hao ndugu zangu mimi nilikuwa ni mdogo wa miaka mitano.
Unaswaga hao wanyama na vumbi lote linakuja kwako. Uso mzima unachafuka vumbi na uonaonekana kama sio mtu, nguo zote zinafanana na vumbi. Hiyo kazi unafanya miaka na miaka lakini huugui. Mahali alipolala ng’ombe na mimi ninalala hapo, ng’ombe akija anakunusa anaona kumbe huyu ni mtu na sio majani anakuacha. Leo ninasema hiyo yote ilikuwa ni neema katika maisha yangu na ndio mana leo ninahubiri.
Hata kama unapita katika changamoto ya aina gani, au jaribu ambalo halieleweki, usiangalie jaribu maana ni sehemu tu ya muda wako wa mafanikio. Unatakiwa kujua ya kuwa “You are going somewhere”. Unaweza kuona mtu amependeza na amekaa lakini hujui alikotokea huko kijijini kwake. Mtu huyu alikuwa anabeba majani, nanakwepa nyoka maporini, na kwa neema ya Mungu nyoka akikuona anakimbia.
Wewe unalindwa na neema ya Bwana, ingekuwa ni zamani ungeshakufa, na kama ni biashara yako ingeshakufa.
Wewe kuna watu wamekutegea sumu na hujajua, kuna matatizo na mitego umewekea na hujajua, lakini neema ya Bwana inakuinua unapanda juu ya matatizo, unajikuta uko ng’ambo. Na mimi ninakutoa unyanyuke juu uende ng’ambo kwa jina la Yesu Kristo.Watu wangeshakumaliza ila neema ya Bwana inakuokoa, inakuponya, inakutoam kwenye shida, kwenye shimo walokuchimbia wakidhani utakufa na wewe unadunda hujafa.
Utaangushwa lakini utasimama, utakataliwa lakini utakubalika. Naomba Mungu leo ukabalike kwa jina la Yesu, kazi yako ikubalike kwa jina la Yesu, uingiapo na utokapo ukubalike kwa jina la Yesu. Sema Fireeee. Unakopitia ni kwa muda dada yangu, hata kama watu hawakuelewi ni kwa muda tu. Yatafika majira watasema, “Heri umebarikiwa kuliko wanawake wote pamoja na uzao wa tumbo lako” Kuna watu hawakuelewi lakini kuna majira watu watakuelewa kwasababu hauko peke yako bali uko na neema ya Bwana, na ndio maana Musa alimwambia Mungu kama neema yako haiku na mimi usiruhusu nigombane na hawa watu unaotaka kuwafuta. Lakini Mungu akamwambia Munsa, “neema yangu haitakuacha”.

Watu watakutukana lakini neema ya Mungu haitakuacha. Wapendwa tupo hapa ni kwa neema tu, maana tulikotoka hakuelezeki, hatuna picha ya kusimama mbele yako, usione Mchungaji wako Lukumay ninaongea ni kwa Neema tu ya Mungu, nilivyo hivi ni kwa neema ya Bwana.

Neema ya Bwana ukiwa nayo hata kama watakutupa jela, watakutendea mabaya lakini Bwana atakuokoa na hayo yote. Ukisoma katika Biblia inasema, walimuwazia vibaya Yusufu lakini aliachiwa Neema. Mtu akiwaziwa mabaya katika vikao vya duniani, basi ujue kikao cha mbinguni kinaanza. Wakichamaliza kikao chao cha duniani cha kukusuta, kukusengenya basi kikao cha mbinguni kinakaa kwaajili yako kukutetea na vikao vibaya vya duniani.
Na mimi ninasema, “Kikao cha mbinguni kikae kwaajili yako, kama ni kikao cha kukuangusha, kikao cha mbinguni kikawe cha kukuinua juu. Watu wabaki midomo wazi wakisema huyu mtu amebarikiwa, na wale wote waliokuwa kinyume chako wakatengenezewe kinyume na kikao cha mbinguni, wale waliotaka ushindwe wakatengenezewe kikao cha ushindi juu yako.  Sema, “ Neema ya Bwana isipungue kwangu, kila ninapoenda, neema Bwana iwe kwangu kwa jina la Yesu”.
Ukisoma kitabu cha Yohana 1:17, Torati na sharia ilikuja kwa mkono wa Musa, lakini Neema na kweli ilikuja kwa mkono wa Yesu Kristo. Mpendwa tusipungukiwe Neema wala kuipuuza. Kukaa katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni “B” ni kwa neema kwani wapo wengi wanatamani kukaa hapa kanisani na kulkalia kiti chako lakini wanashindwa.
Wapo waamini wengine waliokuwepo hapa kanisani wakaondoka na wanatamani kurudi lakini wanaogopa kuja kutokana na aibu walizonazo. Wewe hapo unaneema na unaweza kusalimiana na hata mimi mchungaji wako, lakini wapo wengine wanatamani kusalimiana na mimi lakini wanashindwa kwasababu walichezea neema waliyokuwa nayo na wakaiacha.

Ukiitwa mzee wa kanisa sio kwamba ume - “qualify” ila ni neema tu. Wazee wengine wanaona ni kawaida tu au wameheshimika, hapana ila hiyo ni neema ya Bwana umepewa ya kuwa mzee wa kanisa. Wazee wengine wa kanisa hata ukiangalia “Credit” au “CV” zao za kufungua Biblia, bado hawajui hata kufungua Biblia. Wazee wengine wa kanisa hata ukiwaita kuomba hapa wanashindwa kuomba wanabaki kusema, “Kwa jina la Baba na Mwana na roho Mtakatifu, Amen”, wakitwa kushuhudia utaona matumbo yao yanawaka moto kwa woga.
Kuna watu wanatamani sana kuwepo hapa kanisani Mlima wa Moto Mikocheni “B”. Wapo watu wengine wapo mochwari na hawan, hii Neema, wapo wengine wameshashikwa na hawajapata hii neema, wapo wengine wanatamani kucheza na miguu hawanaa, wengine viuno vyao vimekatika na kutembea kwako mpaka dakika mbili zipite ndio wanweza kunyanyua mguu. Lakini wewe leo hii una neema ya Bwana unaweza hata kucheza kuruka Kimasai halafu bado “Unadengua”, wengine wanasauti nzuri ya kuimba kwaya lakini hawataki kuimba kwaya wanaona wataonekanaje kwa watu wanabaki kusema Yule haimbi vizuri, neema zao wamezificha.
Watu wakishaumwa ndipo wanaanza kujisogeza kwa Bwana wasaidiwe wapone. Lakini mtu mwenye neema akiumwa, Neema ya Bwana inamsaidia na anapokea uponyaji. Ukitaka kuwa na neema ni lazima uwe “mnyenyekevu”. Maandiko yanasema. Methali 3:34. Mungu huwapa neema wanyenyekevu na hawapi wenye kiburi. Kuna watu wengi sana wanapesa nyingi lakini hawana neema ya utoaji. Wengi wanauza vitu vyao lakini hawatoi kwa Mungu, wakishauza wanakumbuka biashara zao na wanasahau malimbuko kanisani.
 
Watu wengine wanakuja kanisani na machenji cheni yao kama sadaka kwa mungu wetu, kwa taarifa yako Mungu hana shida ya chenji, bali Mungu wetu anahitaji heshima. Mungu wetu hana njaa, zaidi zaidi anakusaidia.


 MATUKIO KATIKA PICHA
Mch. Otieno