RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BAHATI AMKARIBISHA WILLY PAUL FOR LUNCH, TEGEMEA NEW JOINT TOKA KWAO

Bahati na Willy Paul Msafi kwa sasa ndio inaaminika wanaongoza kwa sehemu kubwa Gospel Music Industry ya nchini Kenya.Siku chache zilizopita Bahati akiwa na watoto wake alimualika Willy Paul kupata chakula cha mchana kisha kila mmoja wao alipost picha zikiwaonyesha wakiwa pamoja huku Willy paul akisema kupitia page yake ya facebook kuwa “I swear nimeshiba ata siezi amka”Kukutana huku hakukutarajiwa na wengi hivyo kumeleta picha mpya njema kwa muziki wa injili nchini humo.

Bahati kushoto, kulia ni Willy Paul

Hapo nyuma wawili hao walikuwa marafiki sana kabla ya hawajatoka kimuziki lakini baada ya kila mmoja wao kufika juu ghafla kukatokea kutokuelewana kati yao.Msuguano huo ambao wao wanadai ulikuzwa na media ulichangia kwa sehemu kwa wao kuenguliwa kwenye tuzo za muziki wa injili nchini humo maarufu kama Groove Awards 2016.Kuenguliwa huku kulijikita hasa kwenye hoja kuwa kama kweli wawili hawa wanafanya muziki wa Injili kwa nini wachukiane wakati wamezibeba chapa za kristo? Hivyo sababu hii na nyingine ziliwaweka kando kwenye tuzo hizo.

Pichani ni Willy Paul na Bahati wakiwa wamepiga magoti na kupatanishwa kisha wakafanyiwa maombi,hii ilikuwa ni siku ya ufunguzi wa Groove AWARDS 2015

Akizungumza na waandishi wa habari Willy Paul Msafi amesema kwa sasa wanaaangalia namna ya wao wawili kufanya kazi ya pamoja, lengo ni kuupasha umma habari ya Upendo na Amani hususani wale walioamini kwamba kuna chuki baina yao.Lets wait for their new joint