BISHOP DR. GERTRUDE AMWAGIA SIFA ZA KUTOSHA KWA CHRISTINA SHUSHO

Siku ya Jumapili 19.06.2016 katika Ibada ya Kupeleka Waraka Mbele za Bwana iliyofanyika katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B", Bishop Dr. Gertrude Rwakatare alikuwa na haya ya kusema, "Ninayofuraha ya pekee sana kwaajili ya mwimbaji wa nyimbo za Injili Christina Shusho. Amekuwa akihudumu tangia akiwa msicha mdogo. Nakumbuka alivyokuja hapa kanisani kwa mara ya mwisho alikuwa mwembamba sana, lakini ninachomshukuru Mungu ni kwamba bado anaendelea kulinda ushuhuda.Na mimi ninafurahi sana katika huduma yake kuwa “Quality” kwa kila jambo. Yaani ni kama mzungu Fulani, kiatu chake “Quality” nguo yake “Quality”.

Unajua mtu anaweza kujivalia vyovyote lakini Christina Shusho amekuwa akichagua mavazi mazuri kwaajili ya BWANA na yenye heshima. Mungu amempa “shape” na kila kitu, ni mwanamke mzuri, muangalie alivyojisimamisha. Lakini wangekwa watu wengine wangeanza kutikisa miili yao vibaya ili watu washikwe na tamaa ya mapenzi. Mimi nasema usikatike hapa kanisani kakatike chumbani kwako huko na sio hapa madhabahuni.

Mimi ninafurahia sana mtu akiwa “Order”. Nyimbo zake ni nyimbo za kiutu uzima, za heshima, ni tamu na ukicheza hutokwi na jasho"