TANGAZO MUHIMU

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BISHOP DR. M.E. ADMIN

BISHOP DR. M.E. ADMIN

SANDLANDS HOTEL KARIAKOO

BISHOP DR. GERTRUDE RWAKATARE: IBADA YA JUMAPILI 12.06.2016: TENDA MEMA ACHA KUTENDA MABAYA


Bishop Dr. Getrude Rwakatare siku ya Jumapili 12.06.2016 katika ibada ya HABARI NJEMA ndani ya kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni “B” aliweza kufundisha mambo mengi lakini alikazia sana na watu kuacha dhambi na wawe watu wa ktenda mema, alisema. “Ninawasalimu kwa jina la Yesu, naomba tusome Ezekiel 3:6 hata ikawa mwisho wa siku ya saba, Neno la Bwana likaniijia kusema, mwanadamu nimekuweka kuwa mlinzi wa nyumba ya Israel basi sikia Neno hili litokalo katika kinywa changu, ukawape maonyo hayo yatokayo Kwangu. 

Nimwambiapo mtu mbaya hakika utakufa, wewe usimpe maonyo wala husemi na Yule mtu mbaya ilia muonye kusudi aache njia yake mbaya na kuokoa na Roho yake. Mtu huyo mbaya atakufa katika uovu wake lakini damu yake itakuwa mikononi mwako. Tena mtu mwenye haki ukimuonya mtu mwenye ubaya lakini yeye haachi ubaaya wake atawajibika. 

Na mtu mwenye haki akiacha haki yake na kutenda uovu atakufa katika uovu wake wala matendo yake ya haki aliyotenda hayatakumbukwa lakini damu yake nitaitaka mikono mwako kwasababu hukumuonya. Bali ukimuonya mwenye haki kwamba mwenye haki asitende dhambi tena na ikiwa yeye hatendi dhambi hakika ataishi..Bwana Yesu asiiiifiweeee….

TUNATAKIWA KUKAA KAMA WATU WALIOKOKA
Tunatakiwa kukaa kama watu waliokoka. Mimi kama kiongozi wako sitaweza kubadilisha Biblia kama upendavyo eti kwasababu wewe ni dhaifu. Biblia itasimama kama ilivyo, kama Biblia imesema usizini basi na wewe usizini, kama imesema usilawiti basi usilawiti, usiibe basi usiibe. Hakuna mahali utabadilisha Biblia umfae mtu, aliyeshindwa kufuata Biblia kama kanisa tunamtenga tunasema huyu ametenda dhambi. 


Jamani watu wanatuangalia sana sisi tuliokoka katika mitandao, TV na kutusikiliza katika redio. Nakuomab usichafue kanisa zima kwasababu ya udhaifu wako, usiwazuie watu kuja kanisani kwasababu ya kushindwa kwako. Siku za mwisho wanaojitakasa na wazidi kujitakasa, wanaotenda dhambi na wazidi kutenda dhambi lakini nje ya kanisa hili na sio hapa kanisani, ni marufuku.

UNATAKIWA KUWA MLINZI WA NDUGU YAKO ANAPOKOSEA
Neno la Mungu linakupa amri wewe, linasema, “Nimekuweka kuwa mlinzi wa ndugu yako”. Kuwa mlinzi sio lazima umfuate nyumbani kwake, bali unapomuona unatenda jambo baya umuonye, umwambie. 
Wazee unapoona mzee mwenzako anapotoka mwambie mzee mwenzenu, wamama waambie wamama wenzenu, wadada waambie dada wenzenu, vijana waambie vijana wenzenu. Sisi kama watumishi wa Mungu hatuna macho ya kuona kila mahali, lakini tunawaoomba msifunike dambi za watu kwa kubaki kimia bila kuwaonya wanapokosea. 
Wanaotenda dhambi tuwaweke hadharani. Heri kuwa na watu wachache kanisani kuliko kujaza kanisa lenye watenda dhambi ambao hawataki kukosolewa na kutubu dhambi zao. Sasa basi fanya mema na usitendelee kufanya maovu .

Mimi kama Askofu wako Dr. Gertrude Rwakatare sina mbingu ya kukupeleka. Usije ukasema, Bwana Mchungaji au Askofu nipeleke huko mbinguni wakati umebanwa. Ninataka kukuambia kuwa mimi Askofu sina mbingu, ila mbingu ina Mungu, ninachofanya mimi ni kukuonyesha njia ya kwenda mbinguni. Mungu wetu hataki dhambi bali anataka watakatifu.


KWEPA MZIGO WA DHAMBI KWA KUMUONYA NDUGUYO
Jamani wengi tupo katika jijin lenye mambo mengi na changamoto nyingi lakini sisi ni wateule, Bwana ametuchagua katika wengi tumuwakilishe, sisi ni balozi zilizo wazi na zinasomwa na watu wote. Kwa mfano siku ya Alhamisi ya kila wiki watu wanaangalia kipindi chetu cha Faraja Channel Tena, na kuna watu waliokoka na ambao hawajaokoka na wanaangalia kipindi chetu. Kama qwww huq unakaa kwenye kaunta bar na watu wanakuona kuwa umeokoka lakini unapiga moja baribi (bia), jamani hivyo unavyofanya unatuchafua wote sis tuliyeokoka. Acha dhambi, usitende dhambi tena.

Biblia inasema, “Tunawaambia ninyi” Ninyi ni wale waliokoka, washirika, Unapomuona mtu anatenda dhambi na ukanyamaza kimia basi damu yake utadaiwa mikono mwako. Hivi wewe unao haki kweli, ebu jiulize, mtu atende dhambi mwenyewe halafu damu yake udaiwe wewe? Alewe yeye, azini yeye, aibe yeye halafu dhambi zake ziwe mikononi mwako, kwanini? Basi kama unataka kukwepa kubeba mzigo wake wa dhambi, basi umwambie anapokosea, usiogope kukusilika kwake.
Jamani nasema tena uache dhambi kwani mimi sina mbingu ila mbingu ni ya Mungu. 

USIIONEE AIBU DHAMBI
Watu wanaoneana aibu, watu wanasema pembeni, watu wananong’ona, watu wanakonyezana. Haisaidii kukonyezana wala kunong’ona, wala kusema pembeni, ila unatakiwa kusema waziwazi kwa haki. Na hata kama wewe mtenda haki ulikuwa umeokoka na ukapotoka na ukatenda mambo mabaya unatakiwa kutubu. 
Mungu hatakumbuka mambo yako ya zamani, Mungu haangalii mwanzo mwa mtu, Mungu anaangalia mwisho mwa mtu. Unatakiwa kujiuliza unamaliziaje safari yako ya kwenda mbinguni. Umenza vizuri huduma sasa kwanini unajichanganya, kwanini unaharibu kazi ya Mungu. Kwanini unachanganyikiwa, kitu gani kinakuchanganya?

Mimi askofu wako huwa siendi mtaani kuona wewe unafanya nini, ila watu wanaokuona wanakuja kuniambia na kusema, “Mbona huyu mlevi!!!. Nakuomba usitende dhambi tena.

Inawezekana kuishi bila kutenda dhambi. Tunaposema tumeokoka na hatutendi dhambi, sisi hatufekishi (hatudanganyi) ni kweli inawezekana, acha mabo yako yote mtumikie Mungu. Lakini kama unacheza na wokovu ni lazima utatenda dhambi. Kwasababu wazuri ni wengi, vitu vizuri ni vingi, sasa hivi dunia imebadilika na njia za kupata fedha ni nyingi. Unaweza kuchukua “Shortcut” na ukapata fedha lakini kwenda mbinguni huendi.

MTU AKIANGUKA KWENYE DHAMBI AKATUBU ATAINGIA MBINGUNI
Mtu Yule ambaye anamwamini Mungu, na ameanguka na akainuka tena basi huyu ataingia mbinguni lakini ukimwacha utadaiwa damu yake mikononi mwako. Fikiria mtu amekwenda huko na kujichana na kufanya starehe zote na rah azote halafu mwisho wa siku dhambi zake unadaiwa wewe kwasababu hukumuonya, jamani ni haki kweli?

Jamani ninaomba muache dhambi, wakaka muache dhambi,. Dhambi zikija hazina faida, umeng’ang’ania bure. Watu walikuwa na mabaa, watu walikuwa ni maajendi wa kuuza bia lakini waliacha “tender” hizo zote na kumrudia Kristo, waliamua kuja kwa Mungu, waliamua kuacha dhambi. Wakasema heri niishi bila fedha ila waingie ufalme wa Mungu. 
Watu wengine humu wanauza bia kwa siri, huna haja ya kuuza bia kwa siri. Kama umeamua tangaza kweli kuwa wewe huuzi bia au unauza bia. Tangaza msimamo wako ili watu wakuelewe kuwa umeokoka. Tangaza kanisani kwako kuwa umeokoka, tangaza kanisani kwa na nyumbani kwako kuwa umeokoka ili watu wakuelewe.

Nakuomba sasa ujikinge na mauchafu yote, jikinge na marafiki wabaya. Ni heri kuingia mbinguni kibutu au na mguu mmoja kwasababu ukiona mkono wako au mguu wako mmoja unakukosesha basi uukate. Heri kuingia mbinguni na jicho moja. Jicho tunalozumngumzia sio jicho ulinalo bali ni marafiki wabaya, ni heri kuwa bila rafiki na ukawa “antisocial” SIMAMA IMARA NA IMANI YAKO
Mimi hata nikialikwa katika sherehe nikumuona MC anapiga nyimbo za kidunia, huwa ninamwendea na kusema, “naomba uweke nyimbo ya Rose Muhando hasa ule wimbo wa Nibebe” Nachotaka kukuambia ni kusisimama IMARA na IMANI yako. Hata watu wakiniambia nichangie mchango wa harusi, huwa nawaambia pesa zangu zinunue mchele, nyama, soda. Sikubali wachanganye mchango wangu wakanunue bia, huwa naambia wakinunua bia, basi bia zitawapasukia, bia zitapasuka,.

Tunatakiwa kutangaza msimamo mbele ya mataifa, kwani tumekuwa tukiwazuia wengi kuokoka kwasababu ya matendo yaetu machafu, tunajichanganya na mabaya. Ni kitu gani kitakufaidisha katika dunia hii? Jamani ni kitu gani hujawahi kuona, na kama ni starehe si ulishastarehe zamani!! Na BWANA akakutoa huko, sasa kitu ganmi kinakufanya urudi kule tena.

Tunakuomba sana usiwaachafulie wengine wokovu wao. Hili ni kanisa la watu mbalimbali wanakuja kusali, kama umekuja kusali kama dini kwetu ni sawa tu, umekuja kujitakasa kwetu ni sawa tu. Lakini nakuomba sana usiingie katika huduma wakati unaona ulifanya maovu (dhambi). Utakuta mtu yuko “busy” kuchukua kikapu cha sadaka wakati jana alifanya mambo maovu makubwa; ujue unatuchafulia upako wetu.

BISHOP WAKO NINATUKANWA NA WATU ILI WEWE UFIKE MBEINGUNI
Niangalie sana, maana kujenga kanisa hili la Mlima wa Moto Mikocheni “B” ni kazi sana, tunakarabati watu waende mbinguni. Mimi kama Askofu wako, ninabanwa sana, ninasemwa sana, majirani zangu wa hapa kanisani wananisema kuwa napiga makelele, lakini lengo langu ni wewe kuingia mbinguni. Mara nyingine najisikiaga kichefuchefu napoona wewe unajichanganya.

Jamani Mungu awasaidie mtende mema na mbele za watu tuwe ni barua iliyo nzuri, barua inayotia moyo ili watu waingie mbinguni. Pia tunatakiwa kulinda ushuhuda, tusitende dhambi. Ushuhuda maana yake ni kwamba mtu akikuona eneo ulilopo anaanza kukuwazia nini…Mungu akubariki sana.”