MelK Premium Suits

TANGAZO MUHIMU

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BISHOP DR. M.E. ADMIN

BISHOP DR. M.E. ADMIN

SANDLANDS HOTEL KARIAKOO

BISHOP DR. GERTRUDE RWAKATARE: USIKOSE IBADA YA TOFAUTI YA KUOMBEA NYARAKA ZETU JUMAPILI HII YA 19.06.2016 MLIMA WA MOTO MIKOCHENI "B"


Siku ya Jumapili 12.06.2016 Bishop Dr. Gertrude Rwakatare wa kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni “B” alikuwa na haya ya kusema juu ya kipindi cha kufunga na kuomba, ujio wa CROSSOVER mwishoni mwa mwezi Juni 2016, alisema, “Kuanzia Jumatano hadi Ijumaa ya 17.06.2016 itakuwa ni siku za kufunga tatu kavu na kuomba, kutakuwa na ibada ya “Deliverance” kwa siku zote tatu. 
Mwenye mizigo mwenye shida, siku ya Jumatano hadi Ijumaa tutafunga na kuomba ili BWANA aweze kukuokoa katika matatizo uliyo nayo. Tungependa kuwaona wazee, vijana, wanawake,  wanaume wanakuja , wamama, wababa na kila mtu wanakuja.

Ningependa kuwatangazia kuhusu Ibada ya Jumapili 19.06.2016. itakuwa ni ibada ya KUPELEKA MASHITAKA YETU MBELE ZA BWANA, tutapeleka shida zetu mbele za Mungu. Tutasoma Neno la Mungu kutoka katika kitabu cha 2Wafalme 19:4. Siku ya Jumapili utakuja na WALAKA na document zako ambazo zimekufanya usilale usingizi, pengine ni Medical Report ya daktari (madaktari wamesema una ugonjwa mbaya na wamesema upasuliwe, una kansa, una UKIMWI na umekluwa unaogopa na una hofu). 

Pengine unayo barua ya “stop order”, umekuwa ukijenga nyumba yako na umefika kwenye rinda ukapata barua ya “Stop Order”, pengine umepewa barua ya kusimamishwa kazi, pengine umepewa talaka, leta “Driving Licence” yako leta leseni ya biashara yako, leta vyeti vyako vya shule au chuo au kitu chochote kitakachokuunganisha na Mungu kupata mpenyo na Mungu. 
Kwahiyo nasema siku ya Jumapili tutapeleka mashitaka yetu kwa Mungu, na tutaimba “Walaka wa amani”. Kumbuka sisi hatuna waganga, hatuna hirisi wala uchawi ila tunaye Mungu anayetuokoa katika magumu tuliyonayao.
 
Mwisho wa mwizi huu wa sita tutakuwa na “CROSSOVER” na kwa wiki nzima tutakuwa na SEMINA mpaka siku ya IJUMAA ambapo kasha mkubwa utafanyika na akina mama watavaa sare na watu wote watakuja na mishumaa. Siku ya Jumapili kutakuwa na ibada kubwa sana ya kuingia nunsu mwaka kwa KISHINDO nyumbani mwa BWANA. Unajua kila kitu unachofanya ni kujipaisha mwenyewe ili watu wajue, hata harusi yako ukitaka watu wajue lazima uwatangazie. Tunataka huu nusu mwaka iwe ni iezi sita ya ushindi na miezi sita iliyombele yetu iwe ni miezi ya ushindi tukiongozwa na nguvu za Mungu.