RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

HABARI KUTOKA HASSANA KWANZA BLOGU: KUTOKUWEPO KWA TUZO ZA MUZIKI WA INJILI NCHINI, CHRISTINA SHUSHO AWASHANGAA HARRIS KAPIGA, SAMUEL SASALI, JIMMY TEMU, NA HADSON KAMOGA.

Christina Shusho amesema hapa nchini hakuna sababu ya msingi ya watanzania kutokuwa na Tuzo za Muziki wa Injili. Leo asubuhi kupitia kipindi cha Gospel Track cha Clouds Fm kinachoongozwa Harris Kapiga Shuhso amesema wale wadau ambao wako mstari wa mbele kwenye muziki wa injili nchini bado wamelala.Shusho amaesema wadau wote wamezamia kuwa ma Motivational Speakers na Ma Mc badala ya kuiinua industry ya Muziki wa injili nchini.

Christina amesema badala ya kutafuta suluhisho la muziki wa injili nchini wadau wengi wamebaki kutafuta urahisi tu.Akitolea mfano wa wadau wa injili walioko Clouds Media Group (Samuel Sasali, Hadson Kamoga, Harris Kapiga, na Jimmy Temu) amesema wadau hawa wapo kwenye Media inayofanya vizuri sana nchini lakini ninyi mpo tu mmekaa tu mmekalia kuwa ma Mc na ma motivational Speakers aiseeee Bwana awaone”

Harris Kapiga

Muongozaji wa kipindi hicho Harris Kapiga alikubali 100% alichokisema Shusho kuwa ni kweli, Kwa mtazamo wake Harris amesema kikubwa kinachopelekea hali hiyo kwa wadau hao ni kitendo cha kila mmoja wao kutotaka kuwa chini ya mwenzake,yaani kila mtu anafanya vitu kivyake vyake na kutotaka kuwa na kitu cha pamoja.Akitolea mfano wa nchi ya Kenya Shusho amaesema kinachopelekea industry ya Kenya kuwa nzuri ni watu wakawaida ambao wanaadaa matamasha kila weekend.

Hadson Kamoga

Shusho alialikwa redioni na Harris Kapiga kuelezea namna alivyopokea ushindi wake wa Tuzo za Groove awards 2016 ambapo ameibuka kuwa mwanamuziki bora wa nyinbo za Injili kwa nchi za Afrika Mashariki na kati.Sambamba na hilo shuhso ameelezea namna alivyokatisha Ziara yake nchini Marekani iliyodumu kwa siku tatu tu nakurudi nchini Kenya alikoalikwa na Raisi wa Nchi hiyo Mh Uhuru Kenyata katika sherehe maarufu nchini humo za Madaraka’s Day.