RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

HABARI KUTOKA HOSANNA KWANZA: BAADA YA KUSHINDA TUZO YA GROOVE NCHINI KENYA CHRISTINA SHUSHO AMEYASEMA HAYA

Mwimbaji wa nyimbo za injili anaye fanya vizuri Tanzania na Afrika mashariki Christina shusho amesema uwepo wa vyombo vya habari kutosha vinavyo tangaza zadi muziki wa injili nchini Tanzania itasaidia kuongeza idadi ya watu walio okoka na kupunguza idadi ya watu ambao bado hawaja mpokee yesu.

Akizungumza na Hossana kwanza muimbaji wa muziki wa injili ambaye ni mshindi wa Groove awards katika kipengele cha East and central artist of the year 2016 Christina Shusho amesema uwepo wa vyombo vya habari vinavyo saidia muziki wa injili inakuza na kuongeza wigo wa watu kumjua mungu .

Shusho ambaye amekuwa mshindi mara kadhaa wa tuzo za Groove Awards amesema katika mataifa ambayo muziki wa injili unafanya vizuri na watu wengi wanamfahamu Mungu vyombo vya habari vimekuwa chachu kubwa kuutangaza muziki wa injili na injili kwa ujumla.

Aidha Shusho ameshukuru pia wadau mbalimbali wa muziki wa injili ambao wamempigia kura na kumfanya ashinde tuzo hii ya East and central of the year 2016.Amesema anaproject mbalimbali na tayari ameshapata watu ambao watamsaidi kufanya muziki wake ambao anaufanya uzidi kutambulika zaidi kimataifa na sio Tanzania pekee wala Afrika bali Dunia Nzima.

Hata hivyo Amewataka wadau wa muziki wa injili kupokea tena kibao chake kipya kinacho tambulika kwa jina la Unataka akutendee nini ?

Nimekuwekea sauti ya chistina shusho hapa chini akieleza zaidi kuhusu ushindi wake wa tuzo hii ya Groove awards 2016