MelK Premium Suits

TANGAZO MUHIMU

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BISHOP DR. M.E. ADMIN

BISHOP DR. M.E. ADMIN

SANDLANDS HOTEL KARIAKOO

HII NDIO KOLABO YA PILI YA MERCY MASIKA NA WANAMUZIKI WA TANZANIA

Angel Benard toka Tanzania na Mercy Masika kutoka nchini Kenya kwa sasa wako studio wakifanya nyimbo katika studio za Still Alive chini ya Producer TIM wa nchini Kenya.Tim ndiye producer wa nyimbo ya Christina Shusho iitwayo Umenifanya Ning’are, Mwema na Nikupendeze zote za Mercy Masika pamoja na nyimbo nyingine nyingi.Kolabo hii ya Angel na Mercy ni kolabo ya Pili ya Mercy Masika kufanya na watanzania baada ya ile ya Mercy pamoja na Miriam Jackson iliyofanyika mapema mwaka huu na mpaka sasa bado haijaweza kutoka.Hizi zote ni nyimbo za watanzania wakimshirikisha Mercy Masika huenda huko mbeleni tutamuona Mercy Masika akiwashirikisha watanzania.

Ujio wa kolabo hii kwa wawili hawa nje ya kulisambaza neno la Mungu pia utawapa fursa wote wawili kuweza kutanua fun base zao, Ikumbukwe Mercy Masika ambaye ni mshindi wa tuzo nne za injili nchini Kenya(Groove Awards) ikiwa ni pamoja na nyimbo bora ya Mwaka(MWEMA), na Mwanamuziki bora wa Kike nchini Kenya 2015/2016 bado hajafahamika vyema kwa watanzania hivyo itampa kujulikana zaidi nchini. Kwa upande wa Angel Benard ambaye kwa sasa anafanya vyema sana nchini kupitia kolabo hii itampa good platform nchini Kenya na afrika mashariki kwa ujumla.,Hongera sana Angel Benard na Miriam Jackson kwa nia zenu za dhati za kuweza kuiwakilisha vyema Tanzania gospel industry nje ya mipaka yetu.