MelK Premium Suits

TANGAZO MUHIMU

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BISHOP DR. M.E. ADMIN

BISHOP DR. M.E. ADMIN

SANDLANDS HOTEL KARIAKOO

HII NDIO STUDIO YA NNYAKA GOD WIN PRODUCTION, WATU WAZIDI KUMIMINIKA KUREKODI MUZIKI

Tuna kila sababu ya kumshukuru Mungu kwa kuzidi kuwapa watu maono kwaajili ya kuinua vipaji vya watu hususani waimbaji wa nyimbo za Injili Tanzania. Rumafrica inampongeza sana Mkurugenzi wa Nnyaka God Win Production Bwana Godwin L. Maimu kwa hatua aliyofikia kwa kuanzisha studio ya kimataifa. Mungu amemuinua kwa kuwa na producers wazuri wanaojituma kufanya kazi kwa moyo wao wote na kuhakikisha kazi zao zinakuwa "unique" ukifananisha na kazi za watu wengine. 

Waimbaji maarufu sana Tanzania wameanza sasa kukimbilia Arusha kurekodi nyimbo zao kwa viwango vya kimataifa. kama tunavyowaona katika picha, Ann Annie, Stella Joel, Faraja Ntaboba na wengine wengi. Hakika tunastahili kumuunga mkono mtumishi huyu kwa huduma yake hii ambayo itasaidia watu kuwa karibu na Mungu na wengine kuendesha maisha yao kwa kupitia muziki. Hii ni kampuni ambayo itatengeneza ajira kwa vijana na wazee ambao watafanya kazi na Nnyaka God Win Production na Taifa litanufaika na kodi ambayo kampuni hii itakuwa ikiwakilisha katika iadara ya Mapato Tanzania (TRA). 

Tunakuomba wewe mwimbaji kuchukua maamuzi magumu ya kuungana na Nnyaka ili muwezi kufikia hatua ya juu katika ulimwengu wa muziki. Mungu akubariki mmbeba Maono Bwana Godwin L. Maium.
 Faraja Ntaboba kutoka Congo
Ann Annie kutoka Arusha
  Waimbaji NGULI wa nyimbo za Injili STELLA JOEL, FARAJA NTABOBA kutoka Congo,Madame ANN ANNIE, POKEA KAMATA PRODUCER na Mtangazaji REDIO HABARI MAALUM, PAPA TIMOTHEE BULIGA kutoka Congo....wakikaribishwa Mkurugenzi wa NNYAKA PRODUCTION (GOD WIN STUDIO) NA MWIMBAJI WA NYIMBO ZA INJILI TANZANIA NDUGU GODWIN LUDWIG MAIMU (NNYAKA) .