RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

HONGERA CHRISTINA SHUSHO KWA USHINDI ULIOPATA KATIKA GROOVE AWARDS 2016

Mwimbaji wa injili nchini Tanzania Christina Shusho ameibuka kidedea kwenye kinyang’anyiro cha tuzo za groove za huko nchini Kenya kwenye kipengele cha msanii bora wa Afrika Mashariki na kati kwa mwaka 2016.

Shusho amepata tuzo hiyo baada ya kuwashinda kura wapinzani wake kutoka Uganda na Burundi pamoja na John Lisu ambaye pia alikuwa anaiwakilisha Tanzania.

Kilele cha tuzo hizo zimefanyika leo mchana huko nchini Kenya huku hofu kubwa kwa watanzania ilikuwa ni kuwepo kwa waimbaji wawili wa Tanzania kuwepo katika kipengele kimoja lakini mwisho wa siku kura zimeamua.








 















Sio mara ya kwanza kwa Shusho kupokea tuzo za groove na tuzo zingine za kimataifa na inaaminika ndiye mwimbaji wa gospo aliyeipeperusha bendera ya Tanzania kwenye tuzo nyingi za kimataifa.

Uongozi wa GospoMedia unatoa pongezi kwa mwimbaji Christina Shusho kwa kuweza kututoa kimasomaso