MelK Premium Suits

TANGAZO MUHIMU

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BISHOP DR. M.E. ADMIN

BISHOP DR. M.E. ADMIN

SANDLANDS HOTEL KARIAKOO

MAASKOFU KATOLIKI WAMTAKA MAGUFULI KUTUMIA BUSARABARAZA la Maaskofu Tanzania TEC, limemtaka Rais Dk. John Magufuli atende haki na atumie busara na akili anapochukua hatua mbalimbali za utendaji zikiwamo za kupambana na ufisadi.

Kauli hiyo imetolewa na Askofu Msaidizi wa Jimbo Katoliki la Bukoba, Method Kilaini kwa niaba ya TEC, alipozungumza na waandishi wa habari Mwanza.

Askofu Kilaini na wenzake wako jijini Mwanza kuhudhuria kongamano la tatu la taifa la Ekaristi Takatifu litakalofanyika kuanzia Juni 10 hadi 11 mwaka huu.

Akijibu maswali ya waandishi wa habari kuhusu utawala wa Rais Magufuli na matukio yanayojitokeza nchini, Askofu Kilaini amesema taifa lipo katika hofu.

Amesema ni kutokana na matukio ya mauaji yanayofanywa na watu wachache waliokosa hofu ya Mungu na akataka matukio hayo yashughulikiwe kwa uzito unaostahili.

Hata hivyo kiongozi huyo wa kiroho alisema TEC haiwezi kutoa tathmini au kutoa maoni ya uongozi wa Rais Magufuli kwa sasa kwa sababu ni mapema mno.