MelK Premium Suits

TANGAZO MUHIMU

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BISHOP DR. M.E. ADMIN

BISHOP DR. M.E. ADMIN

SANDLANDS HOTEL KARIAKOO

MAMA RWAKATARE KUFANYA IBADA MAALUM JUMAPILI

Stori: Mwandishi wetu, Risasi Jumamosi
Dar es Salaam: Kanisa la Milima ya Moto ‘Mikocheni B Assemblies of God’ linaloongozwa na Mchungaji Kiongozi, Mama Getrude Rwakatare limeandaa ibada maalum kwa ajili ya kukabidhi taifa mikononi mwa Mungu kwa miezi sita ijayo.

Bishop Dr. Gertrude Rwakatare

Kwa mujibu wa Mama Rwakatare, ibada hiyo itafanyika Jumapili ijayo kwenye kanisa hilo lililopo Mikocheni jijini Dar es Salaam kuanzia saa 4 asubuhi hadi saa 7 mchana.

Alisema kuwa ni ibada maalum kwa kuwa waumini watapata nafasi ya kuwaombea viongozi mbalimali, kuwaombea mawaziri, bunge na uchumi wa nchi.

“Kuna mambo kama matatu ya kuombea. Kwanza tutaikabidhi nchi kwenye mikono salama ya Mungu, tutaomba kwa ajili ya vio ngozi, mawaziri, bunge letu na uchumi kwa ujumla,” alisema mama Rwakatare.

Aliongeza kuwa, katika ibada hiyo maalum, pia wenye matatizo mbalimbali wataombewa na kufunguliwa.