RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

VIDEO: SABABU 6 ZA WAPINZANI ZA KWANINI NAIBU SPIKA DR. TULIA AONDOLEWE USPIKA

June 02 2016 Kambi rasmi ya upinzani bungeni imekutana na waandishi wa habari Dodoma ili kuwasilisha mambo makuu sita imetoa sababu kuu sita za kutaka Naibu spika wa Tanzania Dr. Tulia Ackson aondolewe madarakani kwa azimio la kuvunja sheria inayoendesha bunge.

Akiongea kwa niaba ya kambi ya upinzani mbunge wa Simanjiro James Millya amesema >>>’Naibu spika Tulia Ackson ameweka maslahi ya chama chake cha siasa mbele kuliko maslahi ya bunge kinyume na kanuni ya 8 (b) ya kanuni za kudumu za bunge
  1. kutoa uamuzi wa mwongozo ambao ulikuwa unakiuka katiba isemayo kila mtu anastahili heshima ya kutambuliwa na kuthaminiwa utu wake muongozo uliokua unapinga udhalilishaji wa Wabunge Wanawake UKAWA kwamba hawapati Ubunge mpaka waitwe baby, muongozo ulioombwa Dr. Tulia aliudharau’
  1. Tarehe 28 aprili, 2016 alivunja kanuni zinazokataza mbunge kutumia lugha ya matusi kwa         mbunge au mtu mwingine yeyote ambapo alinukuliwa akisema… mheshimiwa Bwege,                     usioneshe ubwege wako humu ndani..
  2. Tarehe 30 May Naibu spika huyohuyo aliamua kwa makusudi kuvunja ibara ya katiba ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania kumzuia Mh. Joshua Nassari kutimiza majukumu yake ya kikatiba ya kuisimamia na kuishauri serikali, ni pale alipoomba muongozo wa jambo la dharura la kufukuzwa kwa Wanachuo wa UDOM, Dr. Tulia alisema hoja hiyo sio ya dharura na wala haikuwa na haja yoyote ya kuwasilishwa.
4. May 26 2016 Naibu spika akiongoza kikao cha bunge bila ridhaa ya kambi rasmi ya upinzani bungeni alishiriki kufuta sehemu ya hotuba ya msemaji mkuu wa kambi rasmi ya upinzani bungeni katika wizara ya elimu kinyume cha kanuni za kuduma za bunge.
5. Kitendo cha naibu spika Dr. Tulia kukataa taarifa tofauti iliyowasilishwa na Wabunge wanne wa upinzani ambao ni Wajumbe wa kamati ya haki, maadili na madaraka ya bunge jambo ambalo ni kinyume cha kanuni ya tano ambapo maamuzi yake haya yalisaidia kuwafukuza Wabunge saba wanaolitumikia taifa hili, adhabu iliyotolewa haikua adhabu inayostahili.