RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

MASTAA WATAKAOBEBA JENEZA LA MUHAMMAD ALI

Bado dunia na mashabiki wa mchezo wa Boxing wapo katika maombolezo ya msiba wa bondia mahiri aliyewahi kushinda mikanda mbalimbali ya Boxing Duniani Muhammad Ali, leo June 7 2016 mitandao mbalimbali imeripo baadhi ya mastaa watakaobeba jeneza la Muhammad Ali.

Kutoka kushoto ni Lennox Lewis alipokabidhiwa tuzo yake ya mwanamichezo bora wa mwaka wa BBC na Muhammad Ali alipopewa tuzo ya heshima ya mwanamichezo bora wa karne 1999

Bondia wa zamani wa uzito wa juu Lennox Lewis ambaye amewahi kushinda mwanamichezo bora wa mwaka BBC 1999 pamoja na Muhammad Ali aliyepewa tuzo ya mwamichezo bora wa karne, ametajwa kuwa miongoni mwa mastaa watakaobeba jeneza la Muhammad Ali.

Kutoka kushoto ni Muhammad Ali enzi za uhai wake na Will Smith

Msanii Will Smith ni moja kati ya mastaa waliotajwa kupewa nafasi ya kubeba jeneza laMuhammad Ali. Muhammad Ali alifariki Ijumaa iliyopita katika hospitali ya Phoenix Arizona akiwa na umri wa miaka 74, lakini taarifa zinaeleza kuwa atazikwa nyumbani kwao Louisville Kentucky.