TANGAZO MUHIMU

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BISHOP DR. M.E. ADMIN

BISHOP DR. M.E. ADMIN

SANDLANDS HOTEL KARIAKOO

MCH. SYLVESTER KOMBA KUTOKA DODOMA ASHANGAZA KANISA LA MLIMA WA MOTO MIKOCHENI "B" JUMAPILI YA UFUNGUZI WA SEMINA YA CROSSOVER 2016

Hii ilifanyika katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" ambapo Bishop Dr. Gertrude Rwakatare na Bishop Danstan Maboya waliweza kufungua rasmi semina hiyo inayoenda kwa jina la CROSSOVER yenye madhumuni ya kumshukuru Mungu kuvuka miezi sita tangia mwaka uanze na kukaribisha miezi sita ijayo kwa maombi ili Mungu alinde safari hii fupi ya kumaliza mwaka 2016. Na siku ya Ijumaa kutafanyika mkesha mkubwa sana wa kuaga miezi sita na kuingia nusu mwaka kwa kishido. Kanisa litapata muda wa kuombea taifa na viongozi wa nchi hii ya Tanzania.

Sasa naomba usikilize ujumbe ambao Mch. Sylvester Komba kutoka katika kanisa la Mlima wa Moto Dodoma alivyoweza kuhubiri siku hiyo ya Jumapili 26.06.2016. Kumbuka semina hii inaendelea mpaka Jumapili hii, na siku za katikati inaanza saa 9 mchana mpaka usiku ila siku ya Jumapili itaanza saa 3 asubuhi.