MelK Premium Suits

TANGAZO MUHIMU

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BISHOP DR. M.E. ADMIN

BISHOP DR. M.E. ADMIN

SANDLANDS HOTEL KARIAKOO

ODAMA: FILAMU ZITATUUA NJAAStori: Boniphace ngumije

MWANADADA anayeuza sura kwenye filamu za Kibongo, Jennifer Kyaka ‘Odama’ amesema kuwa kutokana na namna soko la filamu lilivyododa kwa sasa, kuna kila dalili za wasanii kupigika kiasi cha kufa njaa ikiwa tu hawata jichanganya kwenye michongo mingine.

Akipiga stori na gazeti hili, Odama ambaye filamu yake ya Mkwe iko sokoni aliongeza kuwa tofauti na siku za nyuma ambapo wasanii walikuwa wanatoa filamu sokoni mara kwa mara, wakati huu imekuwa ikiwalazimu kutoa kwa kusikilizia maana hali si nzuri kabisa.

“Soko la filamu kwa sasa limekuwa gumu sana, mtu usipokuwa makini unaweza kufa njaa kama huna michongo mingine, mimi ninafikiri wadau wa filamu wazidi kuwekeza kama wakati wa nyuma ili lirudishe morali,” alisema Odama.